Posts

Showing posts from August, 2017

Shamsa Ford adhamiria kubadilika mana anahisi siku za kufa zimekaribia

STAA wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford amefunguka kuwa, anatamani kumfuata aliyekuwa staa wa Taarab, Mzee Yusuf kwa kuokoka kwani anahisi siku za kufa zimekaribia. Akizungumza na Risasi Jumamosi, Shamsa alisema kuwa, kila kukicha anajikuta anatamani kuokoka na kuacha kila kitu anachokifanya, abaki kusali tu kwani ana hofu sana ya Mungu, lakini hajui ataanzaje, ingawa anajitahidi. “Nimejaribu kusali sala tano kila siku. Kuna wakati ninasahau lakini kuna siku ninasali zote, ninaamini taratibu nitakuwa kama Mzee Yusuf, ninamuomba sana Mungu,” alisema Shamsa.

Messi atupia mbili , Barca ikiua 2-0

Mshambuliaji Lionel Messi akifumua shuti kwa guu la kushoto kumfunga kipa wa Alaves, Fernando Pacheco kuipatia Barcelona bao la kwanza dakika ya 55 katika ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa La Liga Uwanja wa Mendizorroza mjini Vitoria-Gasteiz leo, bao la pili akifunga Muargentina huyo dakika ya 66.

Dc Ally Hapi avutiwa na nyimbo mpya ya Aliliba Seduce Me

Baada ya mwimbaji staa wa Bongofleva Alikiba kuachia video ya wimbo wake mpya ‘Seduce Me’ August 25, 2017, wimbo huo umeonekana kupokelewa vizuri hata na viongozi wa kisiasa ambao hawakuficha hisia zao. Mmoja wa wanasiasa ambao wameonesha kuupokea vizuri wimbo huo ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi ambaye alitumia Instagram yake kuuelezea. DC Hapi aliandika”Nimekuelewa sanaa wajina @officialalikiba. Kazi imeenda shule. Nidai zawadi kwa muziki huu wa ukweli. Keep the fire burning!🔥 #seduceme.”

Anti Ezikieli aigomea ndoa yake

Aunty Ezekiel na mumewe Sunday. DAR ES SALAAM: Siku chache baada ya kuenea kwa madai kuwa mume wa ndoa wa mkali wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel, Sunday Demonte ameachiwa huru huko Dubai baada ya kutumikia kifungo cha miaka kadhaa huku staa huyo akishi kinyumba na mwanaume mwingine, muigizaji huyo amesema ndoa hiyo haipo tena. Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Aunt ambaye alifunga ndoa na Demonte yapata miaka minne iliyopita, alisema kuwa, anawashangaa watu wanaoikomalia ishu hiyo ambayo kwa upande wake ni ndogo. “Ngoja niulize, hivi jamani mbona watu siyo waelewa? Nani asiyejua kama mimi niko na mtu hivi sasa? Na ninaamini kabisa hata yeye (Demonte) anajua? Kwa hiyo hata kama ameachiwa huru na akaja, ukweli utabaki kuwa ndiyo huohuo tu, kwamba tayari nina mtu mwingine maana hata yeye asingeweza kusubiri muda wote huo, hivyo ajue tu hana chake,” alisema Aunt. Staa huyo aliongeza kuwa, kwa hivi sasa ni vigumu kuachana na mzazi mwenziye aliyenaye kwa kuwa tayari wana mtoto am...

Dalili 5 Za Mwanaume Anayekupenda kwa Dhati

Undapo utaona dalili hizi kwa mwezi wako wa kiume basi tambua fika basi, ya kwamba anMapenzi ya kweli. 1. Anakusaidia fedha pale unapokua umekwama kabisa, yuko na jukumu la kukusaidia kiuchumi. Anapenda kukupa kile ambacho amejaaliwa nacho. Hana mkono wa birika, Huyu anakupenda! 2. Anazungumzia future yake na wewe, mipango ya baadae pamoja na wewe, huyu anayo dhamira ya dhati ku Anakupigia simu mara kwa mara na kukuuliza siku yako imeendaje. Anafanya hivi kirafiki na kwa upendo, haigizi. Anakupenda kweli. 3. Anakutembelea mara kwa mara, anakuwa karibu na wewe kipindi unaumwa, hii inamaanisha kwamba yupo tayari kukuvumilia katika shida na raha. Mpende mwanaume huyu. 4. Anawapenda ndugu zako kama ndugu zake. Anaongea nao vizuri na kusaidiana mambo ya hapa na pale. Mtizame kwa jicho la tatu huyu mwanaume! 5. Anaongea na wewe kwa adabu na kwa upole, anakukosoa bila wasiwasi kama kuna mambo unaenenda visivyo. Anakuelekeza njia zilizonyoka..sio wa kumuacha huyu!

Hii Ndiyo Thamani ya kufanya kazi

Kuna tofauti kubwa sana iliyopo kati ya kazi na ajira, unashaanga ndo ukweli huo. Tulio wengi huwa tunazama kazi kama ajira kumbe ni vitu viwili tofauti. katika makala yetu ya leo tutakwenda kuangalia tofauti hizo kati ya ajira na kazi na thamani ya kufanya kazi. Tukianza na kujua maana ya Kazi, kazi ni shughuli yeyote ile iliyo halali au isiyo halali ambayo huifanya mtu kutokana na ujuzi, kibaji na ubunifu ili kupata mapato na faida, ila katika mafanikio tunazungumzia kazi halali tu. Ila ajira ni kile kitendo cha kuuza muda,ujuzi, ubunifu na kumtumikia mwingine, hii hutokea kwa kuwa wewe hujaamua kufanya kazi ya mwenyewe ila umeamua kuajiriwa. Daima tukumbuke ya kuwa kazi ndiyo ambayo inayoanza kabla ya ajira . Ajira ni mizizi ya utumwa nasema hivi nikiwa nina maana ya kwamba kwa kuwa hii karne ya ishiri na moja baadala ya kuwaita watumwa basi wanaitwa wafanyakazi. Leo ingekuwa ni tarehe moja mwezi wa nne ungesema Afisa anaongopa, sijaongopa na huo ndio ukweli usiopingika. kuna baadh...

Mimba kuharibika na Sababu zake

Tatizo la kuharibika kwa mimba limekuwa tatizo kubwa, na limekuwa likiwatesa wengi, kama we ni mongoni mwa watu hao nakusihi usome makala haya ili kuepukana na matatizo haya. Somo hili ni mahususi kwa sababu waawake wengi wamekuwa wakaiharibikiwa na mimba bila kujua sababu. Na zifuatazo ndizo sababu za kuharibika kwa mimba. 1.Mama anapokuwa na matatizo uvimbe (fibroid), huweza kuwa na madhara na kusababisha mimba kuharibika mara kwa mara. 2. Uzito mkubwa (unene) Nayo huweza kuchangia tatizo hilo kinachohitajika ni kuwa na uzito unastahili kulingana na mhusika mwenyewe. Pia inasadikika kuwa uwepo wa manyama uzembe tumboni ni chanzo pia kwa kuharibika kwa mimba kwani, mtoto hukaa kwa shinda. 3. Historia ya kuharibika mimba mara kwa mara Mama aliepata kukumbwa na hali hii ya kuharibika kwa mimba 'miscarriage' zaidi ya mara 2 anauwezo mkubwa wa kuharibika kwa mimba yake kila anaposhika. 4. Utoaji mimba Mwanamke anapotoa mimba mara kwa mara kizazi huweza kuchangia kizazi chake kush...

Manuni 29 za kuishi na Watu/Binadam vizuri

Mojawapo ya mambo muhimu katika mafanikio ya aina yoyote maishani ni kupata msaada wa aina Fulani kutoka kwa watu wengine. Mtu hawezi kufanikiwa bila msaada wa watu,kwa maana hakuna mtu anayejua kila kitu/jambo na anayeweza kufanya kila kitu Duniani. Kwa namna yeyote ile mtu anahitaji msaada wa wengine. Hivyo ili kupata msaada wa wengine ni lazima kujua namna ya kuishi na watu vizuri.Ingawa siyo rahisi kumpendeza kila mtu, lakini watu wengi utaishi nao kwa amani. Zifuatazo ni KANUNI na MBINU mhimu za kuishi na watu vizuri. 1: Uwe na tabia ya kupenda watu kwa moyo wote,hali kadhalika na wewe watakupenda. 2: Heshimu kila mtu na kila mtu umwone ni muhimu sana na wa maana. 3: Usimdharau mtu yeyote kutokana na hali yake,hata akiwa ni masikini ,hakuelimika,hana cheo cha juu na kadhalika. 4: Uwe mtu wa furaha na tabasamu unapokutana na watu. 5: Uwe mcheshi na mtu ambaye watu wanafurahi kuwa nawe. 6: Usipende kulaumu watu na kama utalaumu mtu,tumia njia nzuri na ya upole ya kumsaidia na kumjen...

Ufahamu Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo kiundani

Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni mfumo katika mwili unaohusika na umeng'enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na mwili. Sehemu kuu zinazohusika katika umeng'enyaji huo ni kinywa, umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach', ini, mfuko wa nyongo, utumbo mwembamba 'Duedenum & Ileum', kongosho, utumbo mpana na puru 'Rectum'. Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula hasa kuta za umio, tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na asidi inayotumika kumeng'enya chakula inaposhambulia kuta hizo. Kitaalamu hali hii hutambulika kama 'Peptic ulcers'. Vidonda vya mfumo wa umeng'anyaji chakula vikiwa kwenye tumbo tunaita vidonda vya tumbo 'Gastric ulcer', vikiwa katika duodenum tunaita 'Duodenal ulcer' na vikiwa katika esophagus tunaita 'Esophageal ulcer' VINAVYOSABABISHA VIDONDA VYA TUMBO Bakteria aina ya Helicobacter pylori 'H.pylori' & Non-Steroidal Anti In...

Fahamu Ufugaji wa Nyuki

Kwa kawaida makundi ya nyuki katika nchi ya Tanzania na baadhi ya nchi zinazolingana kwa tabia za nchi, makundi ya nyuki huanza kutafuta sehemu salama na yenye chakula kwa wingi kuanzia mwezi wa kumi katika mwaka mpaka mwezi wa nne kwa mwaka unaofuata.Kipindi hiki huwa na makundi mengi yanayozunguka hapa na pale kutafuta nyumba ambayo itawafaa kwa ajili ya makazi yao na kwa ajili ya kuhifadhia chakula. Hiki ndio huwa kipindi muafaka sana kwa wafugaji kuanza kutega mizinga ambayo imeshaandaliwa kwa ajili ya kufugia nyuki.Kwa kuwa makundi mengi huwa yanatafuta sehemu za makazi hivyo ni rahisi sana kuyakama na kuyahifadhi makundi hayo kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya nyuki. Kutokana na hilo, mfugaji anapaswa kuanza kuandaa sehemu ya kufugiua nyuki na mizinga yake mapema zaidi kabla ya msimu huo kufika ili asiweze kukosa makundi ya nyuki.Unashauriwa kuanza kuandaa mazingira ya kufugia nyuki na mizinga angalau mwezi mmoja kabla kwa kusafisha, kukarabati au kutengeneza kile unachokihitaj...

Lishe ya kuku na kuchanganya chakula

LISHE YA KUKU: Ili kuku waweze kuishi, kukua vizuri, kunenepa na kutaga mayai mengi ni lazima wale chakula kingi na chenye ubora unaotakiwa. Uwingi na ubora wa lishe ya kuku unaweza kuainishwa katika makundi ya vyakula kama ifuatavyo: Vyakula vya kutia nguvu Vyakula vya kujenga mwili Vyakula vya kuimarisha mifupa Vyakula vya kulinda mwili Maji. Makundi ya vyakula: Vyakula vya kutia nguvu: Vyakula vya mifugo vifuatavyo vinawekwa katika kundi hili; Pumba za mahindi, pumba laini za mpunga, na, pumba laini za ngano. Nafaka kama vile mtama , chenga za mahindi ,chenga za mchele, uwele , na ulezi Mimea ya mizizi kama vile muhogo, viazi vitamu na magimbi. Kabla ya kulisha kuku hakikisha mizizi hiyo inalowekwa kwa muda wa saa moja au kupikwa kabla ya kukausha ili kuondoa sumu ambayo kwa asili imo katika vyakula vya aina hii.Inashauriwa kuwa mizizi hiyo ilishwe kwa kiasi cha asilimia 10% ya chakula chote anacholishwa kuku. Katika kundi hili la kutia nguvu ,vyakula vya mafuta kama vile mafuta ya...

Ufugaji wa kuku wa kienyeji kama mradi

MAHITAJI Kuku(tetea) 10 na Jogoo 01 Banda bora Vyombo vya chakula na maji Chakula bora Madawa na chanjo kwajili ya magonjwa Chanzo cha nishati joto na mwanga Elimu na ujuzi wa malezi bora Chombo au chumba cha kutunzia vifaranga Mayai ya kuku wa kisasa/mayai mabovu(ambayo hayakuanguliwa) Madaftari au kitabu cha kutunzia kumbukumbu KUKU 10 Wakati wa kuanza mradi wako hakikisha una kuku 10 (matetea) wenye umri sawa na hawajawai kutaga hata mara moja. Chagua kuku wenye rangi nzuri kutoka katika familia bora kutegemea malengo ya mradi wako. Mfano kama lengo lako ni kuzalisha kuku wa kienyeji kwajili ya nyama basi chagua mbegu ambayo inakuwa haraka na yenye uzito mkubwa. Au ikiwa lengo ni mayai basi ni vema kuchagua aina ya kuku yenye kukua haraka na kutaga mayai mengi. Ili kupunguza gharama za manunuzi ya kuku na hivyo kuongeza faida kwa mfugaji ni vema kununua kuku wadogo ambao wametoka tu kuachishwa kulelewa na mama zao. Kuku hawa utawapata kwa bei ya chini, tena watafaa sana maana wataku...

Uganda:Polisi wawakamata wauaji wa wanawake

Maafisa wa polisi nchini Uganda wanasema kuwa wamewakamata washukiwa kadhaa kufuatia msururu wa mauaji ya wanawake karibu na miji mkuu wa Kampala. Inspekta jenerali wa polisi , Kale Kayihura alisema kwamba mshukiwa mmoja amekiri kuwauawa wanawake wanane kufuatia agizo la mfanyibiashara mmoja. Mauaji hayo yalikuwa ya tambiko fulani kulingana na jenerali Kayihura aliyewaambia wakaazi wa baraza la mji wa Nansana. Vyombo vya habari vinasema wanawake 17 wameuawa katika hali ya kutisha tangu mwezi Mei. Msemaji wa polisi Asan Kasingye aliambia BBC kwamba licha ya mauaji hayo kufanyika katika wilaya moja hayakuwa na uhusiano wowote. Amesema kuwa katika kesi nyingi , waathiriwa walikuwa makahaba ambao walikuwa wamebakwa na kunyongwa katika maeneo yaliotengwa mida ya alfajiri.

Nigeria:Panya wavamia na kuharibu ofisi ya Rais Buhari

Rais wa Nigeria Muhammed Buhari atafanya kazi nyumbani kwa wiki tatu baada ya kurudi nchini humo kufuatia ziara ya matibabu nchini Uingereza. Hii ni baada ya panya kuvamia na kuharibu afisi yake. Msemaji wa rais aliambia BBC kwamba afisi ya Buhari inakarabatiwa baada ya panya kuharibu fanicha na kiyoyozi ndani ya afisi hiyo. Aliongeza kuwa huku ikiwa bwana Buhari hawezi kufanya kazi katika afisi yake kutokana na hali ya afisi yake kwa sasa ,hatua yake ya kufanya kazi nyumbani haitaathiri kivyovyote utendakazi wake kwa njia yoyote. Rais Buhari alirudi nchini Nigeria siku ya Jumamosi , baada ya kukaa mjini London kwa zaidi ya siku 100 ambapo alikuwa akipata matibabu. Amekosolewa katika mitandao ya kijamii kwa kushindwa kuzungumzia kuhusu swala lake la afya katika hotuba kwa taifa siku ya jumatatu. Hii ni baada ya panya kuvamia na kuharibu afisi yake.

Rais wa kwanza wa kosovo afariki dunia

Rais wa kwanza wa Kosovo Bayram Recepi amefariki dunia baada ya kukutwa kapungukiwa damu katika ubongo. Kiongozi huyo amefariki katika moja ya hospitali nchini Uturuki alipokwenda kutibiwa. Kwa mujibu habari,bwana Recepi alikuwa rais wa kwanza wa Kosova mnamo mwaka 2002 mwezi Machi. Recep alisomea udaktari na kuishia kuwa rais wa kwanza wa nchi hiyo kupitia chama cha KDP.

Ibrahimovic akaribia kurudi Man United

UWEZEKANO wa mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic kurejea kazini Manchester United unazidi kuongezeka kutokana na namna ambavyo mchezaji huyo anazidi kuimarika. Mshambuliaji huyo alitemwa kwenye kikosi cha Mashetani Wekundu mwishoni mwa msimu wa 2016/2017 baada ya kuumia, lakini kupona kwake kwa kasi kunazidi kuwaduwaza matabibu wa klabu. Picha zake na video ambazo amekuwa akiposti zikimuonyesha akifanya mazoezi ya aina tofauti yakiwemo ya karate, vinaonyesha ni mtu aliyepona na aliye tayari kurudi uwanjani. Kuna matumaini makubwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 atarudishwa kikosini Manchester United, lakini mshahara wake utaoungua kutoka Pauni 367,640 alizokuwa anapokea kwa wiki wakati anasaini kutoka Paris Saint-Germain mwaka 2016. Matarajio ni kurejea ifikapo January na Ibrahimovic mwenye rekodi ya kufunga mabao 17 katika mechi 27 za Ligi Kuu ya England na 28 kwa ujumla, hajasahaulika na hata wakala wake, Mino Raiola ana matumaini hayo.

Msuva aitakia Yanga ushindi kwenye ngao ya jamii dhidi ya Simba

WINGA wa klabu ya Difaa Hassan El – Jadida amesema anaiamini timu yake ya zamani, Yanga SC inaweza kuibuka na ushindi dhidi ya Simba kesho na anaiombea kwa Mungu ishinde. Yanga SC itamenyana na Simba SC kesho jioni kuanzia Saa 11:00 katika mchezo wa Ngao ya Jamii kuashiria ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Bara msimu wa 2017-2018. Msuva amekuwa mchezaji wa Yanga SC tangu mwaka 2012 alipotua Jangwani akitokea Moro United kabla ya kuuzwa Difaa Hassan El - Jadida mapema mwezi huu. Akiwa na kumbukumbu ya mechi za mahasimu, Msuva ameitakia kila la heri timu yake hiyo ya zamani. “Ninawaamini, na ninawaombea kwa Mungu washinde,”amesema mchezaji huyo wa kimataifa wa Tanzania leo kutoka nchini Morocco. Yanga imerejea Dar es Salaam leo kutoka kisiwani Pemba ilipokuwa imeweka kambi tangu Jumatatu wiki iliyopita ikitokea Zanzibar ilipolala Jumapili baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege, ikishinda 2-0 Uwanja wa Amaan. Na Yanga iliwasili Zanzibar Jumapili ikitokea Dar...

Barcelona yaamua kumshtaki Neymar kwa kuhamia PSG

Barcelona imesema inamshtaki aliyekuwa mshambuliaji wake Neymar kwa kitita cha £7.8m kufuatia uhamisho wake katika klabu ya PSG nchini Ufaransa. Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Brazil alivunja rekodi ya uhamisho kwa kitita cha £200m kwa timu hiyo ya Ufaransa mnamo mwezi Agosti baada ya kununua kandarasi yake katia klabu ya Barcelona . Barcelona sasa inamtaka kurudisha marupurupu aliyopewa baada ya kutia saini kandarasi mpya ya miaka mitano miezi tisa pekee kabla ya kulazimisha uhamisho huo. ''Klabu inataka mchezaji huyo kurudisha marupurupu aliyolipwa kwa kuwa hakumaliza kandarasi yake'', ilisema taarifa. Mbali na Yuro milioni 8.5 za marupurupu, klabu hiyo pia inataka kulipwa asilimia 10 ya fedha hizo kwa kuchelewa kulipwa. Taarifa hiyo iliendelea: Barcelona pia inaitaka PSG kuchukua jukumu la kulipa fedha hizo iwapo mchezaji huyo atashindwa kulipa. Kufuatia uhamisho huo Barcelona ilitangza kuwa inazuilia Yuro milioni 26 za marupurupu ambazo mchezaji huyo alifaa kulip...

Yanga yatua Dar

Kikosi cha Yanga kimetua jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mechi ya kesho dhidi ya Simba. Mechi hiyo ya Ngao ya Jamii inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini. Yanga ilikuwa kambini mjini Pemba kujiandaa na mechi hiyo na msimu mpya wa 2017-18. Hata hivyo, Yanga wamekuwa wakifanya siri sehemu waliyofikia kwa ajili ya kambi ya mwisho kwa ajili ya mechi hiyo.

Tundu Lissu akosa dhamana

Mwanasheria wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amenyimwa dhamana baada ya kukamatwa leo kwa tuhuma za kumkashifu Rais John Magufuli na uchochezi. Akizungumza na Mwananchi leo mwanasheria wake Faraji Mangula amesema kwamba kesho Lissu atapandishwa mahakamani. Amesema Polisi wamedai kwamba amemkashifu Rais a wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Protea. ‘’Polisi wamemnyima dhamana wamesema wanafanya utaratibu wakumfikisha mahakamani’’amesema.

Baada ya Serikali kumnyang'anya mashamba, Sumaye afunguka mazito

Frederick Sumaye. Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania, Frederick Sumaye amesema kunyang’anywa mashamba yake si sababu ya yeye kufikiria kurudi CCM. “Kunyang’anywa mashamba yangu najua ni uamuzi wa juu haunidhoofishi nifikirie kurudi CCM’’ Sumaye amesema mashamba yaliyofutwa na Serikali yalikuwa yanalipiwa kodi na yalikuwa yanamilikiwa kisheria. “Wanataka nirudi CCM, mimi sitaki kurudi CCM, kwanini wananilazimisha? Nilisema sababu za kuondoka huko, waseme wazi sababu za kuyafuta ni za kisiasa tu,” amesema Sumaye leo katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Lissu akamatwa na polisi

Dar es Salaam. Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amedaiwa kukamatwa leo Jumatatu mchana akitokea Mahakama ya Kisutu. Mwanasheria huyo alikuwa na kesi ya tuhuma za uchochezi lakini pia alikuwa ni wakili kwenye kesi inayomkabili mfanyabiashara Yericko Nyerere mahakamani hapo. Akielezea ilivyokuwa Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene amesema wakati gari la Lissu likiwa liko getini tayari kwa kutoka, likazuiwa na nyuma ya gari yake pia likasimama gari jingine likiwa na askari polisi wenye silaha, kisha wengine wakamfuata na kumwambia yuko chini ya ulinzi na atakiwa kwenda Central Police. Wakamtaka ashuke kwenye gari lake na apande gari jingine la kwao kwa ajili ya kuelekea Central Police.

Mwanamke atinga mitaani kutafuta mwanaume wa kumuoa

Mwanamke angia mitaani kumtafuta mwanamume wa kumuoa Nairobi Mwanamke mmoja nchini Kenya ameingia katika barabara za mji mkuu Nairobi, akiwa na bango lenye maandishi yanayosema kuwa anatafuta mwanamume wa kumuoa. Akiwa amevaa nguo nyeupe sawa nguo inayovaliwa Bi harusi, Pris Nyambura mwenye umri wa miaka 28, ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja, alikuwa na bango lililosema. "Ninahitaji bwana, nina mtoto msichana wa umri wa miaka saba"

Alichokisema IGP Sirro kuhusu miili ya Watu kukutwa kwenye viroba katika Fukwe za Bahari ya Hindi

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amezungumzia suala la kuokotwa miili ya watu kwenye viroba katika fukwe za bahari ya Hindi, na kusema suala hilo tayari lipo mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi. Sirro amesema kweli taarifa hizo zimelifikia Jeshi la Polisi, na kwamba tayari miili ipo wenye utambuzi kwa kuchukua vinasaba ili kujua ni raia wa nchi gani, na kisha litatangaza kwa watu walipotelewa na ndugu zao kwenda kuangalia kama ni wao. Kamanda Siro aliendelea kwa kusema kuwa pamoja na kwamba watu wanafikiria mauaji hayo yamefanywa na Jeshi la Polisi, wafahamu kwamba wao kama Jeshi la Polisi huwa hawana kificho, kama wamekutana kwenye mapambano wamewaua watu wataweka wazi kuwa wameua, na siyo kwenda kuwatumbukiza baharini.

Hivi ndivyo Roma alivyomtetea mkewe

Msanii Roma mkatoliki akihojiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo EA Radio amesema aliulizwa ni staili ngapi mkewe amempa, akasema kwa kuwa neno style lina herufi nne basi ni staili nne Alipoulizwa mkewe hajashtuka alipoona post yake imeenea sana, alisema hakuwa na cha kushtuka kwa kuwa hajakosea

Mchezo wa Simba na Yanga ni wa kitoto sana: Masau Bwire

Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema watu hawana raha mitaani kwa kuwa gumzo pekee ni Yanga na Simba kwa kuwa zinakutana kesho. Lakini akasisitiza, timu hizo hazina lolote kwa kuwa zina mambo ya kitoto kwa kuwa huwa hazionyeshi soka lolote zaidi gumzo la mazoea. Yanga na Simba zinakutana kesho kwenye Uwanja wa Taifa katika mechi ya Ngao ya Jamii. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Masau ambaye ni mwalimu kitaaluma, amesema hakuna kipya ambacho timu hizo huwa zinaonyesha. “Nikuambie hawa jamaa hawana lolote hasa kama unazungumzia uwanjani. Mimi naona ni mambo ya kitoto tu, gumzo kubwa kila sehemu mtaani hadi hatuna raha. “Lakini ukienda uwanjani pale, hakuna kiwango chochote kinachoonyeshwa,” alisema.

Yanga kukosa wachezaji hawa dhidi ya Simba

Yanga imethibitisha itawakosa wachezaji wake watatu katika mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba kesho Jumatano. Mchezaji wa kwanza ni ni Obrey Chirwa ambaye anasumbuliwa na kifundo cha mguu na Geofrey Mwashiuya anayesumbuliwa na goti. Pamoja na hao mawinga au viungo wa pembeni, Yanga itamkosa kipa wake Beno Kakolanya ambaye pia anasumbuliwa na bega. Msemaji wa Yanga, Disman Ten amesema, ukiachana na wachezaji hao wengine wote wako fiti kabisa. “Wengine wako katika hali nzuri kabisa na kilichobaki ni suala la mwalimu mwenyewe atasema anamtumia nani,” alisema.

Afrika Kusini:Mawakili kupinga kinga ya kidiplomasia ya Bi Mgabe

Wakili wa Gabriela Engels, mwanamitindo wa Afrika Kusini ambaye alidaiwa kupigwa na mke wa Mugabe bi Grace Mugabe ameambia BBC kwamba atawasilisha ombi katika mahakama kuu mjini Pretoria kukabiliana na kinga ya kidiplomasia iliopewa bi Mugabe. Willie Spies aliambia BBC kwamba mawakili wa bi Engels wanakichukulia kisa hicho kama unyanyasaji kwa lengo la kutaka kumjeruhi mteja wao. Aliongezea kuwa bi Mugabe hafai kupewa kinga hiyo ya kidiplomasia na kwamba serikali ya Afrika Kusini ilikiuka sheria. ''Sheria zetu kuhusu kinga za kidiplomasia ziko wazi. Moja inasema kuwa sheria hiyo haifai kutumiwa iwapo mtu amejeruhiwa na kwamba haifai kutumiwa iwapo uhalifu mbaya umefanyika.Kupiga mtu kwa lengo la kumjeruhi ni uhalifu''. Anasema kuwa mawakili wa bi Engels wataliangazia ombi hilo mahakamani ili kumpa fursa jaji kuweza kubaini iwapo uamuzi huo ulifaa kuchukuliwa ama iwapo unaweza kutengwa.

Amber Lulu afunguka kuhusu Baba yake

Msanii wa bongo fleva Amber Lulu amefunguka na kudai hayamsumbui maneno anayotupiwa na watu mitandaoni kwa yeye kupiga picha za nusu uchi kwa kuwa mtu pekee anayemuhofia hayupo katika mitandao hiyo. Amber Lulu ameeleza hayo kupitia eNewz ya EATV baada ya kuandamwa kwa kipindi kirefu akiwa na watu kuhusu kupiga picha akiwa mtupu na kuweka katika mitandao ya kijamii jambo ambalo lilisababisha baadhi ya watu kudhani mrembo huyo pengine hana wazazi ndiyo maana anajitoa akili kwa kupiga picha za aina hizo. "Dingi nashukuru Mungu siyo mtu wa kufuatilia sana mitandao ya kijamii hasa Instagram 'maybe' aone gazeti na kwenye we abahatishe sana, siyo mtu mfuatiliaji. Kwa hiyo vitu vingi vinakuwa vinapita havijui", alisema Amber Lulu. Pamoja na hayo Amber Lulu aliendelea kwa kusema "Baba yangu anafahamu ninapokaa, siyo kwamba nimetoka huko sijaaga. Niko vizuri yaani nimetoka huko nilipokuwa na baraka zote ndiyo maana naweza kufanya kitu na Mungu naye akaweka baraka zake na n...

Miundombinu ya Gesi asilia kujengwa Dodoma , Mwanza, Tanga, Mbeya na Arusha

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC linakusudia kuanza utafiti wa namna ya usambazaji wa miundombinu ya kusafirishia gesi asilia kwenye mikoa ya Dodoma, Mwanza, Tanga, Mbeya na Arusha. Hatua hiyo inakwenda sambamba na kuandaa mpango kabambe wa mtandao wa miundombinu ya Gesi asilia mkoani Pwani ili kuwezesha viwanda vitakavyojengwa mkoani humo viweze kutumia gesi asilia. Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC Mhandisi KAPUULUYA MUSOMBA wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ziara ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini iliyotembelea eneo la miundombinu ya gesi asilia na ufuaji umeme kwa kutumia gesi asilia lililopo Kinyerezi jijini Dar es salaam. Kwa upande wake serikali imebainisha nia yake ya kuhakikisha viwanda vingi nchini vinaunganishwa na matumizi ya gesi asilia ambapo hadi sasa viwanda 37 vimeshaunganishwa .

Huu ndio uongozi mpya wa Azam Fc

BODI ya Ukurugenzi ya Azam FC imemteua Mwanasheria na msomi, Shani Christoms kuwa Mwenyekiti mpya wa klabu, nafasi iliyooachwa wazi na Nassor Idrissa Mohammed 'Father'. Awali, Shani alikuwa Makamu Mwenyekiti wa klabu na katika mabadiliko haya, nafasi yake inachukuliwa na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Abdulkarim Amin ‘Popat’. Akitangaza mabadiliko hayo mbele ya vyombo vya habari leo, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, alisema kuwa aliyekuwa Mwenyekiti, Nassor Idrissa Mohamed ‘Father’ sasa anakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa bodi. Alisema kuwa bodi hiyo pia imemteua Shani Christoms kuwa Mwenyekiti mpya wa Azam FC, ambaye awali alikuwa Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo. Aidha kwa mujibu wa mabadiliko hayo, nafasi ya Christoms imezibwa na bodi hiyo kwa uteuzi wa Abdulkarim Mohamed Nurdin ‘Popat’, ambaye amewahi kuwa mchezaji wa timu hiyo wakati Azam FC ikiitwa Mzizima. Mbali na kuichezea timu hiyo, pia amesomea mafunzo ya ukocha na mwanzoni mwa mwaka huu a...

Zaidi ya viwanda 42 kuunganishwa mfumo wa Gesi

Serikali imesema kuwa viwanda vingine 42 vitaunganishwa na mfumo wa matumizi wa matunizi ya gesi asilia katika kipindi cha miaka miwili ili kuongeza tija tofauti viwanda 37 vya sasa ambavyo tayari vinatumia gesi hiyo. Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani aliiambia Kamati ya Fedha ya Bunge jana kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa changamoto zinazokwaza zoezi la kuvipatia viwanda nishati hiyo zinatatuliwa haraka. “Tuna gesi ya kutosha futi za ujazo trilioni 57.25 ambapo hadi sasa tunatumia wastani wa futi za ujazo milioni 70 ikiwa ni kama asilimia kumi tu hivi” alieleza Waziri Kalemani.Kwa hivyo alisema azma ya Serikali ni kuona viwanda vinatumia gesi katika uzalishaji na kubanisha kuwa Tanzania inaongoza kwa kuwa na nishati hiyo katika Afrika Mashariki. Waziri Kalemani aliieleza kamati hiyo kuwa hivi sasa wateja wakubwa wa gesi hiyo ni viwanda lakini Serikali ipo mbioni kutekeleza mkakati wa kusambaza gesi hiyo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Katika ...

Hali ya Bulaya bado si nzuri

Dar es Salaam. Hali ya Mbunge wa Bunda Ester Bulaya aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH ) imeelezwa kuwa bado ni tete. Hali hiyo ni kufuatia tatizo la kupumua alilolipata baada ya kuzidiwa akiwa mahabusu ya Kituo cha Kati cha Polisi mjini Tarime. Mwananchi lilifika katika wodi namba 18 Sewahaji alipolazwa mbunge huyo, lakini lilishindwa kuwasiliana naye kutokana na hali yake. Hata hivyo wauguzi wa wodi hiyo hawakutaka kuruhusu mtu yeyote kuingia katika chumba alicholazwa Bulaya. Mbunge wa Kawe, Halima Mdee anayemuuguza kwa sasa hospitalini hapo, jana aliliambia Mwananchi kuwa haiwezekani mtu yeyote kuingia katika chumba hicho kwa sasa. "Hapana hali yake si nzuri kwa sasa hawezi kuingia yeyote huku tafadhali, labda tuombe Mungu kesho hali yake ikiimarika mnaingia," alisema Halima Mdee huku akitoka katika chumba namba 4 alicholazwa mbunge huyo. Akizungumza Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, John Stephen amesema Bulaya alifikishwa hospitalini hapo jana saa tano usiku ...

China kuzindua Treni zenye kasi zaidi dunia kusafiri kwa kilomita 300 kwa saa

Treni za mwendo kasi za China sasa zinatarajiwa kuwa na kasi zaidi duniani. Kasi ya juu ya treni ya kisasa nchini China ilikuwa kilomita 300 kwa saa mwaka 2011 kufuatia ajali mbili ambazo ziliwaua takriban watu 40. Kuanzia wiki ijayo baadhi ya treni hizo sasa zitaruhusiwa kwenda kwa kasi ya kilomita 350 kwa saa. Kasi hiyo ya juu inalenga kupunguza muda wa saa moja kati ya Beijing hadi Shanghai. Kufikia tarehe 21 mwezi Septemba, treni saba za mwendo kasi nchini China zitaruhusiwa kusafiri kwa kasi hiyo ilioongezwa. Ili kuadhimisha kurudi tena kwa treni mwendo kasi, treni hizo sasa zitaitwa ''Fuxing' ama ''zilizoimarishwa'. Treni zote zimewekwa mfumo ulioimarishwa ambao utapunguza kasi ya treni hizo na kuzisimamisha iwapo kutakuwa na dharura . Shirika la treni nchini China linaaminika kutafuta njia za kuimarisha reli ili kusaidia treni hizo kusafiri kwa mwendo wa kasi zaidi wa hadi kilomita 400 kwa saa. China inadaiwa kuwa na takriban kilomita 19,960 ya reli ya mw...

Gambo akabidhi milioni 23

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo leo tarehe 22 Agosti 2017 amekabidhi jumla ya milioni 23 kwa familia za watoto Doreen, Wilson na Sadia ambao walikuwepo nchini Marekani kwa matibabu kufuatia ajali mbaya ya gari waliyopata mwezi wa tano mwaka huu. Mrisho Gambo amepata nafasi ya kukutana na familia za watoto hao pamoja na watoto wenyewe na kudai kuwa kupitia watoto hao na uponywaji wao ameona utukufu wa Mungu "Leo nimekutana na familia za wazazi wa watoto Sadia, Doreen na Wilson ambao watoto wao walinusurika na ajali ya basi ya Lucky Vicent Mkoani Arusha. Aidha, tumewakabidhi 7,750,000 kila familia ili ziwasaidie kwenye masuala yao mbalimbali pamoja na Elimu. Nimeona utukufu wa Mungu kupitia watoto hawa" alisema Mrisho Gambo Watoto Doreen, Wilson na Sadia wamerejea nchini Tanzania kutokea nchini Marekani siku ya Ijumaa ya tarehe 18 Agosti 2017 na kupokelewa na wananchi mbalimbali katika uwanja wa KIA akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na viongozi wengine mbalimbali pamoja ...

Pacquiao kurudiana na Jeff Horn Australia Novemba

IMETHIBITISHWA Manny Pacquiao atakuwa na pambano la marudiano na Jeff Horn mjini Brisbane, Australia baadaye mwaka huu. Tajiri wa Brisbane, Meya Graham Quirk awali alishutumiwa kutoa taarifa bila uthibitisho kutoka kambi ya Pacquiao, lakini sasa amesema kwamba amehakikishiwa hilo katika kikao cha Jumatatu na promota wake. "Nilikuwa na kikao mapema leo (jana) ambacho kimrthibitisha kwamba Manny Pacquiao atakuja mjini Brisbane mwaka huu kwa pambano la marudiano na Jeff Horn," amesema Quirk. Pambano linatarajiwa kufanyika Novemba pale pale Uwanja wa Suncorp ambako watu 50,000 walimshuhudia mwalimu wa zamani wa shule, Horn akimshinda kwa pointi Pacquiao kwenye pambano la raundi 12 kuwania taji la WBO uzito wa Welter. Pacquiao alikataa matokeo hayo akidai mpinzani wake alipendelewa, lakini baadaye likaundwa jopo la wataalamu kupitia upya pambano hilo ili kujua mshindi halali, lakini ikathibitika bondia wa Ufilipino alipoteza pambano kihalali.

Mtuhumiwa shambulio la Barcelona afikishwa mahakamani

WATU wanne wanaoshikiliwa na polisi kwa kushukiwa kuhusika na shambulio la Barcelona, wamefikishwa mahakama kuu ya Madrid kujibu mashitaka yanayowakabili. Pia, mtuhumiwa wa shambulizi la Barcelona, Mohamed Houl Chemlal ni miongoni mwa washukiwa na amefikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kufanya shambulizi lililoua watu 15 na kujeruhi wengine 100. Jaji Fernando Andreu anatarajiwa kuwasomea mashtaka ya kujihusisha na ugaidi, uhalifu na umiliki wa silaha kinyume na sheria. Watuhumiwa hao watabaki rumande kwa muda wote ambao uchunguzi unafanyika. Washukiwa wengine wanane waliuawa, baadhi wakipigwa risasi na wengine wakafa katika milipuko. Kijana mwenye umri wa miaka 22 ambaye naye alikuwa mtuhumiwa shambulio la Barcelona, anayedaiwa kuwa na asili ya Morocco, Younes Abouyaaqoub, anadaiwa kuwa ndiye dereva wa gari lililolipuka na kusababisha vifo na majeruhi hao. Kijana huyo alipigwa risasi na polisi alipokuwa akijaribu kutoroka.

Viongozi wa Serikali mbaroni kwa mauaji ya wanawake watano

Watu 32 wamefikishwa mahakamani kujibu shtaka la mauaji ya wanawake watano yaliyotokea katika Kijiji cha Undomo Kata ya Uchama wilayani Nzega. Miongoni mwa waliofikishwa mahakamani jana Jumatatu na kusomewa shtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nzega, Sarafina Nsana wamo viongozi wa serikali ya kijiji hicho na wengine wa ngazi ya kata. Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Melito Ukongoji aliiambia mahakama kuwa Julai 25, washtakiwa kwa pamoja, wakiwa katika kijiji cha Undomo waliwashambulia kwa kuwapiga na kuwachoma moto hadi kufa wanawake watano kwa tuhuma za imani potofu za ushirikina. Akisaidizana na mwenzake, Agustino Nshimba mwendesha mashtaka huyo aliwataja waliouawa katika tukio hilo kuwa ni Nsuku Masali, Ester Kaswahili, Christina Saidi, Mwashi Mwinamila pamoja na Kabula Kagito. Waliosomewa mashtaka ambao hata hivyo hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza na kuamua mashauri ya mauaji ni pamoja na Mtendaji wa Kata ya Uc...

Umesikia onyo waliotoa Yanga kwa wafanyabiashara?

Klabu ya Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kupitia Afisa habari wake Dismas Ten amewataka wafanyabiashara kuacha kuuza vifaa na jezi zenye nembo za Yanga kuanzia leo na endapo watakaidi agizo hilo watachukuliwa hatua za kisheria dhidi yao. Hayo yameibuka ikiwa imebakia siku moja kuelekea katika mechi ya watani wa jadi inayotarajiwa kupigwa siku ya Jumatano (kesho), ambapo kipindi chote baadhi ya wafanyabiashara huwa wanajipatia kipato chao kwa kuuza jezi za Yanga pamoja na vifaa vingine kwa wachezaji ambao wana lengo la kuingia ndani ya uwanja kutazama mechi. "Klabu inatoa tahadhari (onyo) kwa watu wote ambao kwa namna moja ama nyingine watashiriki kuuza vifaa au jezi zenye nembo ya Yanga SC kuanzia leo, watakamatwa na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao", alisema Dismas katika taarifa yake aliyoitoa. Pamoja na hayo, Dismas aliendelea kwa kusema "kikosi maalum kimeandaliwa kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa jambo hili, na wahujumu wote watakamatwa...

Roma kutinga kwenyee mechi ya Simba na Yanga kesho

Ikiwa imebakia siku kuelekea mtanange kwa mechi ya Ngao ya Jamii, rapa Roma Mkatoliki ambaye ni mshabiki namba moja wa klabu ya Simba amefunguka akidai siku hiyo atakuwepo uwanja wa Taifa kwa lengo la kuwapa hamasa wachezaji na mashabiki wa Simba. Roma amebainisha hayo muda mchache alipotoka katika kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema siku hiyo timu ya Yanga ijiandae kwa kupokea kichapo kitakatifu. "Wanangu wote mashabiki wa timu ya Simba tukutane Taifa kwa ajili ya kumng'oa huyu jamaa wa rangi ya njano (Yanga), tutamkalisha Stamina na wanae wote wanaoshabikia timu hiyo. Najua mashabiki wa Yanga hawataamini kitakachotokea sisi hatuongei sana",alisema Roma. Katika hatua nyingine, msanii Stamina ambaye ni shabiki wa Yanga amedai timu hiyo haina upinzani na klabu yoyote kwa kuwa timu ya Yanga ndiyo imeshikilia rekodi ya ushindi mpaka sasa.

Paparazi akutwa amejinyonga

Mogela Msimbe enzi za uhai wake. Wakazi wa Chalinze na vitongoji vyake mkoani hapa, Jumatano iliyopita walikumbwa na simanzi baada ya paparazzi na mpiga picha wao maarufu, Mogela Msimbe kukutwa amejinyonga kwenye nyumba iliyokuwa ikiendelea kujengwa muda mfupi baada kuaga kuwa anakwenda kushuhudia tukio la wapenzi wawili waliodaiwa kunasiana wakizini ambalo nalo lilidaiwa kutokea siku hiyo. Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliyekataa kutaja jina lake, alisema siku ya tukio marehemu ambaye alikuwa mpiga picha na mwandishi wa habari wa kujitegemea alionekana kuwa na mawazo mengi lakini ghafla zikasambaa taarifa kuwa kuna mwanaume na mwanamke ambao walizisaliti ndoa zao na kwenda kujivinjari gesti, walinasiana wakiwa katika tendo la usaliti. Uvumi huo ulisambaa kwa kasi eneo hilo na kusababisha umati kujazana Kituo cha Afya cha Chalinze, mkoani hapa ambapo watu hao walionasiana walidaiwa kupelekwa kwa ajili ya huduma ya kwanza. “Umati ulizidi kuongezeka k...

Emmanueli Okwi atamba adai hawaogopi Yanga

Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, raia wa Uganda, Emmanuel Okwi amefunguka kwa kujitapa kuwa kuelekea mechi dhidi ya watani wa jadi 'Ngao ya Hisani' kesho atahakikisha anaifunga Yanga japo amepatwa na kitete cha kusema ni magoli mangapi ataifunga. Okwi ameeleza hayo kupitia mahojiano maalum aliyofanya na klabu yake na kusema hawezi kusema ni magoli mangapi atawapachika 'gongo wazi' Yanga kwa kuwa ni klabu ambayo anaiheshimu. "Game ya Yanga siku zote haiwagi rahisi kwa upande wowote kwa kuwa ni timu yenye wachezaji wazoefu wengi japo na sisi tunawachezaji wazoefu wengi kama wao, tunategemea mchezo wa kesho utakuwa mzuri pia tunamatumaini tutashinda", alisema Okwi. Pamoja na hayo, Okwi aliendelea kwa kusema "nitahakikisha timu yangu inashirikiana vizuri na wachezaji wenzangu ili tuweze kutoka na matokeo mazuri katika mchezo huo. Siwezi kusema tutawafunga magoli mangapi kwa kuwa ni timu ambayo ninaiheshimu lakini sisi tutajipanga kuhakikisha tunatoka na m...

Mahakama nchini India yapiga marufuku talaka ya Kiislamu

Five Muslim women moved the Supreme Court to declare instant divorce unconstitutional Mahakama ya juu nchini India imeamua kuwa talaka ya mara moja katika dini ya kiislamu ni kinyume na katiba, uamuzi ambao umekuwa ni ushindi mkubwa kwa haki wanawake. India ni moja ya nchi chache ambapo mwanamume muislamu anaweza kumtaliki mkewe kwa kutamka neno talaq mata tatu. Uamuzi huo wa mahakama unafutia kesi zilizokuwa zikipinga talaka hiyo. Kesi hizo ziliwasilishwa mahakamani na wanawake watano waislamu waliokuwa wamepewa talaka kwa njia hiyo pamoja na na makundi mawili ya kutea haki. Miaka ya hivi karibuni visa vingi vimeibuka ambapo wanaume waislamu huwataliki wake zao kwa kutamka neno talaq mara tatu, kwa njia ya simu au kwa kutuma ujumbe ya sms, kupitia WhatsApp na Skype. Licha ya njia hiyi ya kutaliki kutumiwa kwa miongo kadha hiajatajwa popote pale kwenye Sharia au Koran

Wasioendana na kasi ya Rais Shein watakiwa kuacha kazi

Kauli hiyo ameitoa mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi kisiwani Zanzibar Ayoub Mohamed Mahamoud mbele ya Waandishi wa habari kuwa kwasasa Serikali yake ya mkoa haitaweza kumvumilia mtumishi yeyote ambaye hatatekeleza majukumu yake kwa weledi na kwa wakati na hivyo kuwataka wajitathmini wenyewe. "Nataka nieleze, kwa watendaji ambao wanaona hawaendani na kasi yangu na ya Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein waanze kuachia ngazi wenyewe... Hatutaweza kumvumilia mtu yoyote anayekwamisha" Alisema RC Ayoub Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Rais Shein kutoa maagizo 13 kwa mkuu huyo wa mkoa na kuhakikisha yanatekelezwa kwa wakati. RC Ayoub amesisitiza kuwa kila kinachofanyika kwasasa ni lazima kiende kwa kasi na kwa kiwango cha juu. Kwa mujibu wa mkuu huyo wa Mkoa ofisi yake sasa inaanza mchakato kutathmini ili kubaini watendaji hao mara moja. Mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi kisiwani Zanzibar Ayoub Mohamed Mahamoud

Peter Msigwa amtolea uvivu Msukuma, ampa makavu

Mbunge wa Iringa mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa ameibuka na kumchana Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku na kusema uelewa wake juu ya hoja za Mwanasheria Tundu Lissu ni mdogo sana. Msigwa amesema haya siku moja baada ya Mbunge Msukuma kudai kuwa yeye anaunga mkono kauli ya serikali kuhusiana na wanasiasa kuchochea sakata la ndege huku akiwatuhumu kuwa wapinzani wanatafuta kiki na kusema ni waongo watupu. "Msukuma anasukumwa na uelewa Mdogo wa mambo ya kisheria na kimataifa kwa uelewa wake juu ya hoja za Tundu Lissu ni sawa na kobe kushindana na twiga kwa uwezo wa kuona Mbali" alisema Peter Msigwa Aidhaa Mchungaji Msigwa ameitaka serikali kutoa majibu yanayoridhisha kuhusiana na ndege inayoshikiliwa nchini Canada "Hoja zilizotolewa na Serikali juu ya kukamatwa kwa ndege yetu huko nchini Canada Bombadier Q 400 zinafedhehesha Taifa na kuondosha weledi na umahiri wa Serikali katika kukabiliana na maswala makubwa ya nchi yetu. Kinachoshangaza S...

Mwili wa mwanaharakati wa Tembo kuagwa leo

Wayne Lotter enzi za uhai wake. MWILI wa mwanaharakati wa kupinga ujangili na biashara haramu ya meno ya tembo wa nchi za Afrika Wayne Lotter, aliyepigwa risasi na kuuawa jijini Dar es Salaam Jumatano iliyopita unatarajiwa kuagwa leo katika viwanja vya Baobao Villlge Masaki jijini Dar. Wayne ambaye alikuwa mwanzilishi wa PAMS Foundation, taasisi ambayo imekuwa katika mstari wa mbele kusaidia kupambana na uwindaji haramu na biashara ya pembe za ndovu nchini Tanzania aliuawa na watu wasiofahamika Agosti 16 mwaka huu wakati anatoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere akielekea nyumbani kwake Masaki. Akizungumza na wana habari kwa niaba ya wana familia, jana Krissie Clark alisema wanatarajia kuuaga mwili wa mwanaharakati huyo leo kisha kuusafirisha kwenda nyumbani kwao Afrika Kusini kwa maziko. Alisema kuuawa kwa Wayne hakutawafanya kurudisha nyuma mapambano dhidi ya ujangili na badala yake wameelekeza nguvu zao katika Afrika ili kutokomeza kabisa ujangili kama ilivyokuwa ndoto ya ndugu yao...

Washtakiwa kwa kula nyama ya binadamu Afrika Kusini

Wanaume 4 washtakiwa kwa kula nyama ya binadamu Afrika Kusini Wanaume wanne wamefikishwa kwenye mahakama ya Afrika Kusini kujibu mashtaka ya ulaji nyama ya binadamu, baada ya madai kuwa mmoja wao alifika katika kituo cha polisi na kusema kuwa amechoka kula nyama ya binadamu. Alipohojiwa zaidi mwanamume huyo alionyesha sehemu ya mguu na mkono wa binadamu. Kisha polisi wakaandamana na mwanamume huyo hadi kwa nyumba moja iliyo mtaa wa KwaZulu-Natal, ambapo sehemu zaidi za miili ya binadamu zilipatikana. Wanaume wanne, wawili kati yao madaktari wa kitamaduni walikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji au kupanga kuua. Walifikishwa katika mahakama ya Estcourt kilomita 175 kaskazini magharibi mwa mji wa Durban. Msemaji wa polisi aliiambia BBC kuwa kuna uwezekano kuwa wanaume hao wanne walio na umri wa kati ya miaka 22 na 32 ni sehemu ya genge kubwa. Uchunguzi bado unaendelea na polisi wamewashauri watu ambao jamaa zao wametowewa kujitokeza. Wachunguzi wa visa vya uhalifu wameitwa kutambua sehemu hi...

Trump aapa kuwa atashinda vita hii

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani kutoka nchini Afghanistan kutaacha pengo ambalo huenda likajazwa na magaidi. Alisema kuwa mapango yake ilikuwa ni ya kuondoa vikosi vya Marekani, lakini badala yake ameamua wanajeshi hao kubakia ili kuzuia kurudia makosa ambao yalitokea nchini Iraq. Amesema pia kuwa anaongeza idadi ya wanajeshi watakao pelekwa nchini Afghanstan. Akizungumza kupitia Televishen, Rais Trump amesisitiza kuwa kipaumbele cha Marekani ni kutekeleza masuala yenye maslahi katika usalama wa taifa hilo, kutokomeza mtandao wa ugaidi. Amesisitiza pia kuwa kitendo cha Marekani kujiondoa kwa haraka Afghanistan, kitatatoa mwanya kwa ugaidi kujiimarisha zaidi kama ilivyotokea Iraq. Hata hivyo Trump amekwepa kuzungumzia moja kwa moja muda wa mwisho wa ushiriki wa Marekani nchini Afghastan na idadi kamili ya ongezeko la wanajeshi. Rais Trump ameitupia lawama Pakistan kwa madai kuwa inawahifadhi magaidi ambapo amesema suala hilo linapaswa kuac...

Tshishimbi amkuna Lwandamina Zanzibar

TSHISHIMBI. LICHA ya kiungo mpya wa Yanga, Papy Tshishimbi, kuchelewa kuanza kufanya mazoezi ya pamoja na wenzake, kocha wa klabu hiyo, Mzambia George Lwandamina, amesema amevutiwa na mwanzo wake mzuri na kufafanua kuwa atakuwa msaada kwao. Lwandamina alililiambia Nipashe jana kuwa, nyota huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameonyesha kujituma katika mazoezi visiwani Zanzibar tangu alipojiunga rasmi na timu hiyo hivi karibuni. “Bado hana muda mrefu ndani ya kikosi, lakini kwangu naona ameanza vizuri na amekuwa mwepesi kushika maelekezo na kuzoea wenzake,” alisema Lwandamina bila kuweka wazi kama atamuanzisha mchezaji huyo kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba itakayopigwa Uwanja wa Taifa kesho.

BMT yashikilia rungu mabadiliko Simba Sc

KATIBU MKUU WA BMT, MOHAMMED KIGANJA. SIKU moja baada ya wanachama wa Simba kuridhia mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji katika klabu yao, Baraza la Michezo Tanzania (BMT), limesema linasubiri taarifa rasmi ili liweze kutoa mwongozo ndani ya klabu hiyo. Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja, alisema taarifa za Simba kufanya mkutano huo wanazifahamu na ofisi yake ilizikaimisha kwa Msajili wa Vyama na Klabu za Michezo nchini. Kiganja alisema kuwa anaamini viongozi na wanachama wa klabu hiyo watakuwa wamefanya uamuzi kwa kuzingatia katiba. "BMT kwa sasa hatuwezi kusema chochote kuhusiana na kilichopitishwa katika mkutano huo wa jana (juzi), mpaka tutakapopata taarifa rasmi ya kile kilichoamuliwa na wanachama hao, mimi nimesikia kupitia vyombo vya habari ambavyo kila kimoja kimeandika kulingana na mrengo wake," alisema Kiganja. Wanachama 1,216 kati ya 1,217 waliokutana juzi walikubali kwa kauli moja kuuza asilimia 50 ya hisa kwa mwekezaji yeyote au ...

Wakimbizi mbaroni kisa fujo kambini

JESHI la polisi Mkoa wa Kigoma, linawashikilia wakimbizi 19 wa Kambi ya Nduta iliyopo Wilaya ya Kibondo kwa tuhuma za kufanya fujo. Kamanda wa polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui, alisema vurugu hizo zilidumu kwa takribani saa sita kambini hapo jana. Kamanda Mtui alisema wakimbizi hao walifanya fujo wakitaka kuvamia na kuvunja ghala la chakula la Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula (WFP). Alisema wakimbizi hao waliziba barabara kisha kuharibu miundombinu mbali mbali ya shirika hilo wakiwa na lengo la kuchukua chakula kutoka ghalani wakidai kuwa chakula walichopewa ni kidogo na hakitoshi. Kwa mujibu wa Kamanda Mtui, kufuatia vurugu hizo askari walijipanga vyema kwa kuimarisha ulinzi ikiwamo kufanya doria katika kambi hiyo na kufanikiwa kuwadhibiti. Alifafanua kuwa ni askari wake pia walifanikiwa kuwakamata wakimbizi 19 ambao wanatuhumiwa kuwa chanzo cha fujo hizo. Kamanda Mtui alisema upelelezi wa tukio hilo unaendelea ili kuwabaini watuhumiwa wengine waliohusika na tukio...

Mwalimu Afikishwa Mahakamani kwa kumbaka Mwanafunzi na kumjaza mimba

Mwalimu wa shule ya msingi katika kata ya Ligunga tarafa ya Matemanga wilaya Tunduru mkoani Ruvuma Rajabu Morisi amefikishwa katika Mahakama ya wilaya hiyo kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake na kumsababishia ujauzito. Akisoma shauri hilo no 148/2017, mbele ya mlinzi wa amani hakimu wa Mahakama ya mwanzo Itika Korosho, mwendesha mashtaka wa Mahakama ya wilaya Inspekta Bosco Kilumbe amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo kati ya mwezi January na Mei mwaka huu katika muda usiojulikana baada ya kumrubuni mwanafunzi huyo. Na kudai kufanya hivyo ni kinyume cha sheria namba 130 (1) na (2e) na namba 131 (1) na (2) vya sheria ya kanuni ya adhabu sura namba 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002. Hata hivyo mtuhumiwa huyo amekana kosa hilo upelelezi bado unaendelea , mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana, kesi hiyo itatajwa tena Mahakamani Agosti 28 mwaka huu.

Daktari feki wa Muhimbili anaswa tena Hospitali ya Amana

Mkaazi wa jiji la Dar es Salaam, Abdallah Juma aliyewahi kukamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akidaiwa kujifanya daktari amenaswa tena katika Hospitali ya Rufaa ya Amana kwa kufanya kazi katika hospitali hiyo wakati sifa za udaktari hana. Juma alinaswa jana ndani ya Hospitali ya Amana, majira ya mchana, akijifanya daktari, baada ya kuwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo. Kukamatwa kwa Juma kunakuja ikiwa ni miezi mitatu tu imepita tokea Juni 19 mwaka huu alipo kamatwa katika hospitali ya Muhimbili kwa kujifanya daktari. Katika hospitali ya Muhimbili kijana huyo alijifanya kutoa huduma katika maabara kuu huku uongozi ukiwa hauna taarifa ya kuwepo kwa huduma aliyokuwa akiitoa kitu ambacho kilisababisha kushtukiwa na kukamatwa. Baada ya kukamatwa Uongozi wa hospitali hiyo ulifanya uchunguzi na kubaini kuwa kijana huyo hakuwa daktari bali daktari feki kama alivyokuwa akijitambulisha na kwamba amekamatwa mara baada ya kuwekewa mtego na askari wa hospitali hiyo. Daktari w...

Mechi ya Simba na Yanga kuanza saa 11 jiini

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema mechi ya watani Yanga na Simba, itaanza saa 11 jioni. Awali mechi hiyo ya Ngao ya Jamii, ilipangwa kuanza saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, keshokutwa Jumatano. Lakini Msemaji wa TFF, Alfred Lucas ametangaza mabadiliko hayo ya ratiba ya mchezo huo kusogezwa kwa saa moja zaidi.

Tshabalala sasa yuko fiti kabisa

Cosmas Kapinga ambaye kwa sasa ni meneja wa Simba, ametoa ufafanuzi kuhusiana na ile ishu ya taarifa za Mohammed Zimbwe ‘Tshabalala’ kuzimia takribani dakika tatu uwanjani wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Gulioni. Kapinga ambaye kitaaluma ni daktari, amesema Zimbwe alianguka na kupata maumivu makali ya bega hivyo kumfanya aonekana kama ambavyo waandishi walianza kuamini alizimia. "Alikuwa na maumivu makali sana ya bega, hakuzimia dakika tatu kama ilivyoelezwa. Lakini alilazimika kutulia kwa muda wakati akipata matibabu. "Unajua kama mchezaji atazimia dakika tatu, basi atatakiwa kupumzika kwa siku sana. Lakini unamuona Tshabalala yuko na wenzake. "Nafikiri waandishi walipaswa kuwa makini zaidi katika kuangalia hilo," alisema Kapinga. Kwa maelezo hayo ya Kapinga, maana yake Zimbwe yuko fiti kabisa na itakuwa ni uamuzi wa mwalimu Joseph Omog acheze au la. Taarifa za awali zilieleza hivyo, kuwa Zimbwe alizimia wakati wa mechi hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya m...

Wachezaji Yanga na Simba kupimwa kama wanatumia Madawa

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema wachezaji wote watakaochezwa mechi ya Ngao ya Jamii ya watani Yanga na Simba, watachukuliwa vipimo. Lengo la TFF ni kuwapima wachezaji wote ili kuangalia kama kuna wale wanaotumia madawa haramu ya kuongeza nguvu. Msemaji wa TFF, Alfred Lucas amesema lengo lao ni kuufanya mchezo kuwa fair kiuchezaji na anayeshinda, ashinde kwa haki. “Hata hivyo hatujasema kwamba kuna timu fulani wachezaji wake wanatumia dawa, badala yake hii ni katika kujiridhisha tu,” alisema. Tayari TFF imetangaza kuwa mechi hiyo ya Ngao ya Jamii, itaanza saa 11 jioni ikiwa imesogezwa mbele kwa saa moja. Simba waliweka kambi Unguja na Yanga wako Pemba na sasa kinachosubiriwa ni “Show Time”.

Roma Mkatoliki atoa siri ya Zimbabwe

Rapa Roma amedai sababu za kusema anakwenda Zimbabwe ni kutokana na ukweli kwamba nchi hiyo ni moja kati ya nchi ambazo ziliguswa na matatizo aliyopata ikiwepo kutekwa na kuteswa kwa siku tatu mfululizo. Akizungumza leo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Roma amesema ingawa tayari idea ya wimbo huo ilikuwepo lakini alitamani kuonyesha mama wa Afrika kwani Zimbabwe ni kati ya nchi ambazo Tanzania ilisaidia kutafuta uhuru wake. "Ningeweza kwenda Zimbabwe au nchi nyingine yoyote Afrika lakini nilitaka kuonyesha Mama wa Afrika, ukizingatia Rais Mandela na Nyerere tayari wameshaondoka lakini Mugabe yupo hai. Nilipopata matatizo watu wa nchi mbalimbali walipaza sauti zao ili tuliokuwa tumetekwa tupate kurudi tukiwa hai, kwa hiyo nikaona bora iwe Zimbabwe ingawa tayari idea ya wimbo huu ilikuwepo muda mrefu kidogo" Roma. Pamoja na hayo Roma amefunguka na kusema wanaodhani kuwa Zimbabwe ni kubwa kuliko ngoma zake zote wanakosea kwani wakati alipoingia kwenye game wimbo wake w...

Rais Buhari atoa hotuba ya kwanza baada ya kurejea Nigeria

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameihutubia taifa baada ya kuwa Uingereza kwa miezi mitatu akipata matibabu. Katika hotuba yake kwenye televisheni, Buhari, mwenye umri wa miaka 74, alisema "alifadhaishwa" na wito wa kuigawanya Nigeria, akiwahimiza Wanigeria kuwa na umoja. Lakini rais hakufichua anaugua wapi. Hii ilikuwa mara yake ya pili kuchukua likizo kwa sababu za kimatibabu mwaka huu. Raia wengi wa Nigeria walimwomba ajiuzulu wakati hakuwepo nchini, wakisema hakuwa na uwezo wa kuiongoza nchi. Wengine wamemuuliza kusema anaugua nini huku uvumi ukiongezeka kuhusu uwezekano wake kuwania urais tena mwaka 2019. Makamu wa Rais Yemi Osinbajo amekuwa akiwajibika wakati Buhari amekuwa Uingereza, lakini Buhari sasa amerejelea kazi yake kama rais. Akizungumza siku mbili baada ya kurudi kwake, Buhari alisema kuwa maoni kuhusu kuwaganywa kwa Nigeria "yamevuka mstari wa rangi nyekundu". "Umoja wa Nigeria upo na sio wa kujadiliwa," alisema. "Hatuwezi kuruhusu ...

Mke wa Roma. Naahidi kukupa style zote

Mke wa msanii wa Roma, Nancy ametoa ahadi yenye utata kidogo kwa mumewe mara baada ya video yake ‘Zimbabwe’ kufikisha views milioni moja. Siku ya jana August 20, 2017 video ya Roma ilifikisha idadi hiyo ya views katika mtandao wa YouTube tangu ilipoweka katika mtandao huo August 10 mwaka huu. Kitendo hicho kilimchanganya Baby Mama huyo na kukimbilia katika mtandao wa Instagram na kuandika ujumbe mfupi; Finally You Made It #1Milion_Views Ndani ya Week 1 Na siku 3!!!😘😘 Walahi Mume wangu @roma_zimbabwe#LEO_NITAKUPA_STYLE_ZOTE Kwa Furaha Niliyonayo!!! Hongera Mno!! Much Congrat kwa shemela @nicklassm Nakuona Mbali Saaana!! Video hiyo hadi sasa ina views 1,040,849, hata hivyo imetoa katika trending baada ya kukaa katika number one trending kwa wiki moja. Lakini video mpya ya Rostam (Roma & Stamina) ‘Hivi Ama Vile’ ameanza kufanya vizuri ambapo kwa sasa inashika nafasi ya tatu katika trending.

Shinikizo la damu. Chanzo na Tiba yake

Nini maana ya shinikizo la damu? Ni msukumo wa damu ulio juu kuliko inavyotakiwa kwa muda mrefu. Msukumo wa damu huhitajika mwilini ili kusambaza chakula, oksijeni na kutoa uchafu. Shinikizo la damu hupimwa kwa kutumia kifaa kinachoitwa Sphygmomanometer Shinikizo la damu husababishwa na nini? Vitu vifuatavyo vinaweza kusababisha shinikizo la juu la damu: Uvutaji sigara Unene na uzito kupita kiasi Unywaji wa pombe Upungufu wa madini ya potassium Upungufu wa vitamin D Umri mkubwa Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin) Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin Uanishaji wa shinikizo la damu Presha ya kawaida

Tatizo la ugumba kwa wanawake

Ugumba ni hali ya mwanamke kushindwa kushika ujauzito. Linaweza kuwa tatizo pia kwa mwanaume lakini katika makala hii tutaona nini kinasababisha tatizo hili kwa upande wa wanawake. Nini husababisha ugumba kwa wanawake? Mayai kutokomaa ipasavyo: Tatizo la mayai kutokukomaa vema ndilo chanzo na sababu kuu ya wanawake wengi kushindwa kushika ujauzito na hii inachukua karibu asilimia 30 ya wanawake wote wagumba. Habari njema ni kuwa tatizo hili linaweza kurekebishwa kirahisi ikiwa mwili utapewa vile viinilishe mhimu vinavyokosekana hadi kupelekea mayai kutokomaa vizuri. Vinavyosababisha mayai ya mwanamke kutokomaa vema: (1) Matatizo ya kihomoni Matatizo katika homoni ndicho chanzo kikuu cha mayai kutunga bila kukomaa vizuri. Hatua za ukomaaji wa mayai zinategemea uwiano mzuri wa homoni na namna zinavyotegemeana katika kufanya kazi. Jambo lolote linalovuruga homoni kubaki katika uwiano wake sawa na wa kutegemeana na wenye kufanya kazi ipasavyo linaweza kupelekea utungaji wa mayai ambayo ha...