Posts

Showing posts from October, 2017

Mvua kubwa zatarajiwa kunyesha usiku wa leo

Image
Dar es Salaam.  Mamlaka ya Hali ya Hewa(TMA) imetangaza vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya masaa 24 vinatarajiwa kuanza usiku wa kuanzia leo Jumanne. Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo Jumanne imeeleza kuwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam na Pwani pamoja visiwa vya Unguja na Pemba yataaririka. “Mvua hiyo inatarajiwa kusambaa katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Lindi kuelekea siku ya Ijumaa ya tarehe 3 Novemba 2017.” “Hali hii inatokana na kuwepo na kuimarika kwa ukanda wa mvua (Inter Tropical Convergency Zone –ITCZ) katika maeneo hayo.” Mamlaka hiyo imewataka wakazi wa maeneo yaliyotajwa kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zinazotolewa “Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo kila itakapobidi.”

RC Makonda anusuru zaidi ya Tsh bilioni moja

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo amekabidhi Mabasi 10 chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kampuni ya DAR COACH LTD kwaajili ya kufufuliwa upya na kuwa ya kisasa. Mabasi hayo 10 chakavu yanatoka kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Magari 3, Jeshi la Polisi Magari 4 pamoja na Jeshi la Magereza Magari 3 ambapo yote kwa pamoja Matengenezo yake yameokoa kiasi cha Shilingi Billion 1,110,000,000 ya Serikali. RC Makonda amesema kuwa Gari hizo zitatengenezwa na kukamilika ndani ya Siku 90 ambapo ameipongeza Kampuni ya DAR COACH LTD kwa kujitolea kukarabati Magari hayo bila kutumia pesa ya Serikali. Aidha Makonda amesema Magari hayo yatafungwa Vifaa vya Kisasa ikiwemo Kiyoyozi (AC), Mfumo wa Chaji ya Simu kila Seat, Runinga, Radio, Viti vya kisasa, Vyoo vya Ndani, Bodi mpya pamoja na mwonekano mzima wa Gari ili ziwe za kisasa. RC Makonda amesema mpango wake wa kuendelea kuongezea nguvu Vyombo vya Ulinzi na Usalam...

Aslay anunua BMW

Image
Msanii wa muziki wa bongo fleva Aslay Isihaka ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Natamba' amefunguka na kushukuru uongozi wake mpya kwa kufanikisha yeye kuweza kupata ndinga mpya aina ya BMW. Aslay ambaye ndani ya muda mfupi ameweza kuachia nyimbo zaidi ya 10 na ngoma hizo nyingi kufanya vizuri na kupokelewa vyema na wananchi jambo ambalo limeweza kufungua milango kwa msanii huyo kuweza kupata show nyingi na mafanikio mbalimbali. "Alhamdulillah Asantee Mungu kwa hiki ulichonipa naishukuru management yangu Chambusso na Mxcarter, nakupenda Mama yangu kokote ulipo kila hatua dua 'new car' Umma unaongea" alindika Aslay kupitia mtandao wake wa Facebook. Aslay Isihaka kwa mara ya kwanza kuanza kumiliki gari yake alizawadiwa na uongozi wake wa kwanza wa Yamoto Band chini ya Mkubwa Fella katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake mwaka 2015.

Halima Mdee afunguka kuhusu bunge

Image
Mbunge wa Kawe kupitia CHADEMA Halima James Mdee, amesema mambo yanayoendelea nchini yamechangiwa na kutokuwa na bunge imara, ambalo linashindwa kuwawajibisha viongozi wanapokwenda kinyume. Halima Mdee ameyasema hayo alipokuwa akiongea na mwandishi wa East Africa Radio, na kusema kwamba hata Spika anayeliongoza Bunge hilo hana uamuzi huku akishindwa kuchukua uamuzi kadri mamlaka ya bunge yanavyomtaka.

Meya wa Jiji la Mwanza afunguka

Image
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire amefunguka juu ya sababu zilizomfanya akamatwe na polisi wakati wa msafara wa Rais Magufuli alipokuwa Mwanza. Akizungumza na waandishi wa habari Meya huyo amesema sababu ya kukamatwa kwake alielezwa ni amri kutoka kwa viongozi wa juu ili asiwepo kwenye msafara wa Rais, na kupata fursa ya kuzungumza yale ambayo anayajua. Meya Bwire ameendelea kwa kusema kwamba katika jiji hilo kuna vitendo vya matumizi mabaya ya fedha pamoja na kudhulumu haki za wananchi, na kamwe hatoacha kuzungumza hata kama anahatarisha kibarua chake.

Simba yampa Omog nafasi nyingine

Image
Pamoja na taarifa kuendelea kuzagaa kwamba Kocha Joseph Omog kiota kimeanguka, Kamati ya Utendaji ya Simba imekutana na kukubaliana Kocha Joseph Omog kuendelea kukinoa kikosi hicho. Omog amekuwa katika hali ya hatihati kama vile atafukuzwa kazi kutokana na mwenendo wa timu yake. Lakini taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza, katika kikao hicho wamekubaliana Omog kuendelea na kazi yake. “Lakini ametakiwa kubadili mambo na kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa, Simba inataka ushindi,” kilieleza chanzo. Mwenendo wa Simba katika mechi nane ilizocheza imekuwa ni milima na mabonde kwa kupitia ushindi, sare, ushindi sare. Hali hiyo imesababisha kuwepo kwa taarifa nyingi ambazo zinaeleza kwamba Omog anakaribia kutimuliwa. Hata hivyo, bado hali inaonekana kuwa haijatulia na Omog atalazimika kufanya kazi ya ziada kuhakikisha anabadili mambo.

Yanga kumkosa Juma Abdul kwenye mechi dhidi ya Singida United

Image
Wakati Yanga itakuwa na kibarua cha kuivaa Singida United kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida, wikiendi hii, taarifa za uhakika zinaeleza, itamkosa beki wake wa kulia, Juma Abdul. Abdul ana kadi tatu za njano, ya mwisho akiwa ameipata katika mechi dhidi ya Simba, Jumamosi. "Juma ana kadi tatu, kadi ya tatu ameipata dhidi ya simba baada ya kupata nyingine dhidi ya Kagera. Hivyo hatacheza mechi ya Singida," taarifa zilieleza. Hakuna mtu wa benchi la ufundi la Yanga alipatikana kuzungumzia baada ya simu zao kuwa zinaita bila majibu. Lakini taarifa nyingine zikaeleza kuwa, tayari Yanga wana taarifa kuhusiana na Juma Abdul. "Hatakuwa katika mipango ya safari, benchi la ufundi linajua Juma ana kadi tatu."

Mavugo akalia kuti kavu Simba

Image
Viongozi wa Simba wameonyesha kutofurahishwa na uchezaji wa mshambuliaji wao Laudit Mavugo hasa kutokana na kushindwa kuonyesha juhudi uwanjani. Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza, viongozi wa Simba wamemtaka Mavugo kujituma na kama inashindikana basi wataachana nao. "Viongozi hawajafurahishwa na Mavugo kwa kuwa hajaonyesha juhudi zozote katika mechi dhidi ya Simba. "Unajua hata katika upangaji, awali kocha alionekana kama nafasi ya kuanza angempa Bocco. Lakini alibadili ikawa ni Mavugo," kilieleza chanzo. "Viongozi wao hawana uwezo wa kumuingilia kocha lakini wanakerwa na namna Mavugo asivyoonyesha kama ana uchungu. Hivyo walitaka kama ameshindwa aende zake. "Tayari kaelezwa kuwa lazima ajitume na acheze kuitumikia timu na kuisaidia kwa kuwa kama ilivyo kwa wengine anapata kila kinachotakiwa."

Lissu afunguka kuhusu Nyarandu

Image
Dar es Salaam.  Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema), Tundu Lissu amempongeza aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki(CCM), Lazaro Nyalandu kwa kupata ujasiri wa kuchukua hatua kubwa ambayo hata wabunge wengi waliopo ndani ya CCM wanashindwa kuichukua. Lissu ambaye yuko kwenye matibabu jijini Nairobi  amempongeza Nyalandu kwa kuwa ni alikuwa mbunge jirani yake na kuwa ujasiri wa kufanya hivyo. Mbali na kumpongeza Nyalandu pia Lissu amezungumzia  uchaguzi wa madiwani katika kata 43 akieleza kuwa kuwapa CCM kura katika kata hizo ni sawa na kukubaliana na yanayoendelea nchini. “Kuwapa CCM kura sasa hivi ni sawa na kuwapa CCM mamlaka ya kutapanya mali zetu kama wanavyotaka,”amesema Lissu leo Jumanne akiwa jijini Nairobi.

Haji Manara avutiwa na mbinu za kocha wa Yanga

Image
Ni mara chache sana kusikia kiongozi au hata shaki wa Simba na Yanga kusifia timu pinzani kutokana na utamaduni wa vilabu hivyo ulivyo hata kama watatakiwa kupongeza, leo October 31, 2017 Haji Manara amesema waziwazi kukubali mbinu zilizotumiwa na kocha wa Yanga George Lwandamina kwenye mchezo wa Yanga vs Simba Jumamosi iliyopita. Manara amesema Lwandamina ni mtu wa mbinu na alifanikiwa katika mbinu zake za kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza ambapo  timu hizo zilitoka sare ya kufungana 1-1, Simba walianza kupata goli la kuongoza lakini Yanga wakasawazisha dakika mbili baadaye. “Yanga walicheza vizuri tena kwa nidhamu, kocha wao ni mtu wa mbinu sana alikuja kupaki ‘basi’ kwa heshimba ya kuiheshimu Simba lakini akazitumia vizuri ‘counter attack’, walicheza vizuri bila shaka kwa sababu walikuja kama underdogs wakatuheshimu, wakapaki basi lao vizuri.” Manara amewaambia Yanga kwamba, kushangilia kwao matokeo ya sare ya 1-1 yanadhihirisha Sim...

Zitto Kabwe ameachiwa huru

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameachiwa huru kwa dhamana na kutakiwa kuripoti siku ya Jumanne saa tatu asubuhi kwa Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI) jijini Dar es Salaam. Mwanasheria wa Zitto Kabwe amesema kuwa mpaka sasa mteja wake anatuhumiwa kwa makosa mawili tofauti likiwepo kuchapisha taarifa kinyume cha sheria ya mitandao lakini kosa jingine ni kutoa takwimu za uongo kinyume na kifungu cha 37 (5) cha sheria ya takwimu ya mwaka 2015 hivyo mwanasheria anasema Zitto Kabwe amehojiwa na kutoa maelezo yake hivyo wanasubiri kujua kama watakwenda mahakamani. Kwa upande wake Zitto Kabwe amefunguka na kusema kwa sasa wanasubiri kuona wanapelekwa mahakamani ili waweze kujadiliana huko na kusema kama wao kuna makosa ambayo wanayaona kwake sehemu pekee ambayo wanaweza kwenda kufafanua vizuri ni mahakamani na kudai kuwa kama asingekamatwa angeshangaa kwa kuwa tayari Rais alikuwa ameshatoa agizo. "Tunasubiri ni lini watatupeleka mahaka...

CHADEMA Yajitoa uchaguzi wa Naibu Meya Kinondoni

Image
Dar es salaam.  Chadema imesema haitashiriki uchaguzi wa naibu meya unaotarajiwa kufanyika katika Manispaa ya Kinondoni. Katibu Mkuu wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo leo Jumanne Oktoba 31,2017 ameieleza Mwananchi kuwa, baada ya kikao cha madiwani wa mkoa na baadhi ya viongozi wamekubaliana kutoshiriki uchaguzi huo. Uchaguzi wa naibu meya hufanyika kila mwaka nchini ikiwa ni utekelezaji wa sheria. "Hatutashiriki kwa sababu tulifungua kesi Mahakama Kuu inayopinga uhalali wa Meya wa Kinondoni, kwa hiyo kushiriki itakuwa ni kuhalalisha tunachokikataa mahakamani," amesema. Kilewo amesema wiki iliyopita ofisi yake ilipokea barua kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa manispaa hiyo, Aron Kagurumjuli ikitaka kupendekeza jina la mgombea wa nafasi hiyo kabla ya Oktoba 30,2017. Akizungumzia kauli ya Chadema, Kagurumjuli amesema hakuna barua aliyoipata kuhusu uamuzi huo. Amesema ofisi yake imepokea jina la mgombea wa CCM leo Jumanne Oktoba 31,2017 na inasubiri vyama ...

Manara:Tulinyimwa penati mbili dhidi ya Yanga

Image
KLABU  ya Simbe imelalamika kunyimwa penalti mbili na refa Hery Sasii katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga SC uliomalizika kwa sare ya 1-1 Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Sunday Manara amesema refa alikwenda na matokeo yake uwanjani. Manara aliwawekea Waandishi wa Habari video ya mchezo huo kuwaonyesha namna ambavyo refa Sasii hakutoa penalti licha ya mpira kuwagonga mikononi beki, Kevin Yondan na kiungo Mkongo, Papy Kabamba Tshishimbi Jumamosi. Manara aliyewabeza watani wao hao wa jadi, kwamba ni kawaida yao kupendelewa na marefa kila wanapokutana na Simba amesema watapeleka malalamiko Bodi ya Ligi dhidi ya refa huyo na wengine walioionea timu yao katika mechi zilizotangulia. Akasema huo ni mwendelezo wa matukio ya klabu yake kutotendewa haki na marefa katika mechi za L...

Harry Kane yupo fiti kuivaa Real Madrid kesho

Image
Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa mazoezini na wenzake leo baada ya kupona maumivu ya nyama za paja wakijiandaa na mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya kesho dhidi ya Real Madrid Uwanja wa Wembley, London.

Raila Odinga asema hawautambui uchaguzi wa Uhuru Kenyatta

Image
Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Nasa Raila Odinga ameapa kuendelea kufanya maandamano dhidi ya uchaguzi wa Uhuru Kenyatta akisisitiza kuwa upinzani haumtambui. Odinga anasema kuwa Nasa haitambui uchaguzi huo kwa kuwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati pamoja na kamishna aliyejiuzulu Roselyn Akombe walithibitisha kwa umma kuwa tume hiyo haiwezi kusimamia uchaguzi ulio huru kutokana na misimamo ya kimapendeleo ya baadhi ya makamishna katika tume hiyo. Odinga ambaye alikuwa akitoa mwelekeo wa upinzani kwa vyombo vya habari katika jumba la OKoa Kenya jijini Nairobi amesema kuwa ana ushahidi wa kutosha kwamba kulikuwa na uingiliaji na uongezaji wa kura katika ngome za chama tawala cha Jubilee. Anasema kwamba iwapo uchaguzi huo utaruhusiwa na kutambulika utawavunja moyo Wakenya wengi na hivyobasi kuwafanya kutoshiriki katika uchaguzi mwengine wowote. Mr Odinga pia amesema kuwa hawezi kuwaruhusu watu wawili wanaojigamba kuwa na uwezo kuharibu uhuru na demokrasia ilipatika...

Zitto Kabwe afunguka baada ya kuachiwa

Image
Dar es Salaam.  Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema asingekamatwa na polisi angeshangaa. Amesema hilo linatokana na kauli ambazo zilitolewa na baadhi ya viongozi wa Serikali kuhusu takwimu alizotoa. "Kila mtu alijua tutakamatwa na kama tusingekamatwa basi tungeshangaa,” amesema Zitto leo Jumanne Oktoba 31,2017 baada ya kuachiwa kwa dhamana na polisi. Zitto amesema maelezo ya kina na ufafanuzi wa kauli zake zinazodaiwa kuwa za uchochezi atayatoa atakapofikishwa mahakamani. Ufafanuzi mwingine anaodai atautoa atakapofikishwa mahakamani ni kuhusu masuala ya takwimu na makosa ya mtandao. Pia, amewataka wanachama wa ACT Wazalendo kuendelea na shughuli zao kama kawaida na hasa katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani utakaofanyika Novemba 26, 2017. Zitto baada ya kuachiwa, mwanasheria wake Stephen Mwakibolwa amesema akiwa Kituo cha Polisi Chang'ombe, mteja wake  alihojiwa kwa kosa la uchochezi alilolifanya wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani...

Rais Magufuli awapa siku 14 wamiliki wa viwanda

Image
Rais John Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa kiwanda cha nguo cha Mwatex cha jijini Mwanza na cha dawa cha Keko jijini Dar es Salaam kuonyesha mpango madhubuti wa kiutendaji na uendeshaji. Amesema kinyume cha hilo, viwanda hivyo vitataifishwa na kurejeshwa kwenye umiliki wa umma. Rais Magufuli amesema hayo leo Jumanne Oktoba 31,2017 alipozungumza na wananchi baada ya kuzindua kiwanda cha dawa za binadamu cha Prince Pharmaceutical eneo la Buhongwa jijini Mwanza. Amesema Serikali imechoka kusikia kauli na maelezo ya “tuko kwenye mchakato” zinazotolewa kama kinga kwa viwanda visivyofanya kazi kwa kiwango kinachostahili. Rais ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kuwa kiwanda cha Mwatex kinafanya kazi kwa asilimia 20 ya uwezo wake wa uzalishaji. Akizungumzia ujenzi wa kiwanda cha dawa, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema utawezesha mikoa ya Kanda ya Ziwa kuwa na uhakika wa upatikanaji wa dawa kwa bei nafuu. Mwalimu amesema katika utekelezaji wa Tanzania ya viw...

Msigwa:Nyarandu amewaonyesha Watanzania mambo saba muhimu

Image
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Peter Msigwa amefunguka na kumpongeza Lazaro Nyalandu na kumwambia kuwa amechukua uamuzi sahihi kuachana na chama hicho na kusema amewaonyesha watanzania mambo saba muhimu. Msigwa amesema kitendo cha Nyalandu jana kuamua kuachana na Chama Cha Mapinduzi ni wazi kuwa amethibitisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) si chama tena bali kimekuwa chini ya dola na hakina uwezo wa kuikosoa serikali tena. Msigwa aliainisha mambo hayo saba kama ifuatavyo 1. Nyalandu umethibitisha kwamba CCM sio Chama Cha siasa tena. CCM iko chini ya miguu ya dola na haina uwezo wa kuikosoa serikali tena 2. CCM imepoteza mwelekeo wake. Imeshindwa kusimamia uchumi, siasa na uongozi wa nchi 3. Misingi ya nchi yetu imebomolewa chini ya utawala wa CCM na umeitisha mwito wa kila mmoja wetu kuijenga upya misingi ya nchi yetu 4. Tanzania imekithiri ukiukwaji wa haki za binadamu , dhulma na kutekwa na serikali mhimili wa bunge pamoja mahakama. 5. Watanzania wapate fursa ...

Ccm kupeleka vijana Ulaya

Image
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetoa fursa ya kuwapeleka barani Ulaya vijana watakaochaguliwa na shirikisho la soka nchini Tanzania TFF kwaajili ya kupata mafunzo ya kuchezesha soka. Hilo limedhibitishwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho ndugu Humphrey Polepole kwenye mahojiano na eatv.tv ambapo amebainisha kuwa fursa hiyo imetolewa na vyama rafiki vya chama hicho kwenye nchi za Ulaya. Polepole amesema kupitia kikao kikubwa cha vyama vyote vya kijamaa barani Afrika na Ulaya kilichofanyika mapema mwaka huu ilitolewa fursa kwa CCM kuweza kupeleka vijana kwenye baadhi ya nchi barani Ulaya ili kupatiwa mafunzo hayo. Aidha Polepole amebainisha kuwa zoezi hilo litasimamiwa na TFF kwasababu wao ndio wana dhamana ya kupitisha watu wanaohusiana na soka hivyo watashirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha vijana wanatumia fursa hiyo ambapo baada ya mafunzo hayo watarudi kuitumikia sekta ya michezo nchini.

Baada ya kuona ameolewa mume wake amejibu mapigo

Image
Aliyekuwa mume halali wa muigizaji wa filamu bongo Irene Uwoya, mcheza soka kutoka nchini Burundi Hamad Ndikumana, ameonyesha kujibu mapigo baada ya mwenza wake kuonekana kuolewa, kwa kupost picha akiwa na mwanamke mwengine. Kwenye ukurasa wake wa instagram Ndikumana amepost picha hizo, huku akiandika ujumbe kama ambao unaonekana ni kurusha vijembe kwa mwenza wake huyo, ambaye hivi karibuni alimuandikia waraka kuanika yale aliyokuwa akithubutu kuyafanya, na kusema yuko tayari kutoa talaka. Wawili hao walitfunga ndoa takatifu katika kanisa la Mtakatifu Joseph la Jijini Dar es salaam, na kutengana baada ya muda mfupi wa ndoa yao, huku kukiwa na tetesi kuwa hakuna maelewano baina yao. Tazama mapicha aliyopost Ndikumana

Muigizaji akiri kushiriki mapenzi ya jinsia moja

Image
 Muigizaji mkongwe kutoka Uingereaza Kevin Spacey amefunguka kwa mara ya kwanza na kukiri kushiriki mapenzi ya jinsia moja. Kevin ambaye ni maarufu pia katika tamthilia ya ‘House of Cards’ ameamua kutoa kauli yake baada ya muigizaji na msanii wa muziki Anthony Rapp kudai kuwa amekuwa akisumbuliwa na Spacey toka aliwa na umri wa miaka 14, wakati huo Kevin ana miaka 26. Kauli ya Rapp(46) imetoka wakati akifanyiwa mahijiano na Buzzfeed, Hata hivyo Spacey(58) amefunguka na kuadai kuwa alimuomba radhi kijana huyo na kumtaka asionge ila anashangazwa na Rapp kuamua kusema sasa.

Ajibu ajazwa zawadi jangwani

Image
Mwigizaji na msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi maarufu kama ‘Ray’, amewaongoza mashabiki wa Yanga SC kutoka kundi la ‘Yanga For Life’ kwenye mtandao wa WhatsApp kutoa zawadi kwa wachezaji wa timu hiyo. Ray na wenzake wametoa zawadi ya fedha, viatu na ‘Shin Gard’, mchana wa leo kwa wachezaji watatu, waliofanya vizuri katika michezo ya Ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu. Miongoni mwa wachezaji waliopata zawadi hizo ni mshambuliaji Ibrahim Ajib ambaye amepewa kiasi cha Tsh Milioni moja, baada ya kuibuka nyota wa mchezo kwenye mechi mbili za Kagera Sugar na Stand United. Kiungo kutoka DRC Papy Kabamba Tshishimbi, ambaye aliibuka nyota wa mchezo wa watani wa Jadi jumamosi iliyopita amepewa zawadi ya shilingi laki tano huku kipa Youthe Rostand, akipata shilingi laki mbili, viatu na ‘Shin Gard’.  Baada ya kukabidhi zawadi hizo Ray amesema nia ya kundi lao ni kuwapa hamasa wachezaji wao ili waweze kutetea ubingwa wao wa ligi na k...

Rais Magufuli afunguka mazito kuhusu wanaohama CCM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa wapo watu ambao walikuwa ni wezi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema saizi watu hao wamekimbilia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Rais Magufuli amesema hayo leo Oktoba 31, 2017 akiwa ziarani mkoani Mwanza ambapo alikuwa akiongea na wananchi wa Mkuyuni na Butimba jijini Mwanza na kusema kuwa yeye anataka maendeleo kwa kuwa anaamini Tanzania inahitaji kujengwa na Watanzania wote na kudai ndani ya vyama vya siasa kuna wezi ambao hao ndiyo wamechelewesha maendeleo ya nchini. "Tunataka Tanzania mpya hilo ndiyo lengo langu kwa sababu yapo yalikuwa ni majizi makubwa sana Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakakimbilia CHADEMA ndiyo maana sijasema CUF oyeee kwa sababu wapo waliomo CUF wengine ni wabaya sana. Mimi nataka maendeleo kwa sababu maendeleo yanaletwa na Watanzania wote tushikamane ndugu zangu tutachelewa tushikamane sasa hivi tuipeleke Tanzania yetu mbele" alisisitiza Rai...

Nyarandu amechukua maamuzi sahihi amethibitisha CCM Si Chama tena , Peter Msigwa

Image
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Peter Msigwa amefunguka na kumpongeza Lazaro Nyalandu na kumwambia kuwa amechukua uamuzi sahihi kuachana na chama hicho na kusema amewaonyesha watanzania mambo saba muhimu. Msigwa amesema kitendo cha Nyalandu jana kuamua kuachana na Chama Cha Mapinduzi ni wazi kuwa amethibitisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) si chama tena bali kimekuwa chini ya dola na hakina uwezo wa kuikosoa serikali tena. Msigwa aliainisha mambo hayo saba kama ifuatavyo 1. Nyalandu umethibitisha kwamba CCM sio Chama Cha siasa tena. CCM iko chini ya miguu ya dola na haina uwezo wa kuikosoa serikali tena 2. CCM imepoteza mwelekeo wake. Imeshindwa kusimamia uchumi, siasa na uongozi wa nchi 3. Misingi ya nchi yetu imebomolewa chini ya utawala wa CCM na umeitisha mwito wa kila mmoja wetu kuijenga upya misingi ya nchi yetu 4. Tanzania imekithiri ukiukwaji wa haki za binadamu , dhulma na kutekwa na serikali mhimili wa bunge pamoja mahakama. 5. Watanzania wapate fursa ...

Mahakama yamkuta Scopion na kesi ya kujibu

Image
 Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemkuta mshtakiwa Salum Njwete, maarufu kwa jina la ‘Scorpion’ anayekabiliwa na shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi ana kesi ya kujibu na anatarajiwa kuanza kujitetea, Novemba 14, mwaka huu. Uamuzi huo umetolewa leo Oktoba 31/2017 na Hakimu Mkazi Flora Haule wa mahakama hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na zaidi ya mashahidi kumi  walioletwa mahakamani pale na upande wa Mashtaka. Kabla ya kutolewa uamuzi huo, Hakimu Haule alimkumbushia mshtakiwa mashtaka yake.  Baada ya uamuzi huo kutolewa, mshtakiwa Scorpion amedai kuwa atajitetea kwa kiapo na pia atakuwa na mashahidi wawili ambao walitoa ushahidi upande wa mashtaka. Hata hivyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili Ester Kyala ulipinga hoja hiyo na kudai kuwa mshtakiwa huyo hawezi kutumia mashahidi ambao wamekwisha toa ushahidi wao kwa upande wa Jamhuri na kama anaweza atafute mashahidi wengine. Kutokana na pingamizi hilo Scorpion amed...

Msigwa ampongeza Nyalandu kuhamia CHADEMA Ataja mambo saba yaliyomvutia

Image
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Peter Msigwa amefunguka na kumpongeza Lazaro Nyalandu na kumwambia kuwa amechukua uamuzi sahihi kuachana na chama hicho na kusema amewaonyesha watanzania mambo saba muhimu. Msigwa amesema kitendo cha Nyalandu jana kuamua kuachana na Chama Cha Mapinduzi ni wazi kuwa amethibitisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) si chama tena bali kimekuwa chini ya dola na hakina uwezo wa kuikosoa serikali tena. Msigwa aliainisha mambo hayo saba kama ifuatavyo 1. Nyalandu umethibitisha kwamba CCM sio Chama Cha siasa tena. CCM iko chini ya miguu ya dola na haina uwezo wa kuikosoa serikali tena 2. CCM imepoteza mwelekeo wake. Imeshindwa kusimamia uchumi, siasa na uongozi wa nchi 3. Misingi ya nchi yetu imebomolewa chini ya utawala wa CCM na umeitisha mwito wa kila mmoja wetu kuijenga upya misingi ya nchi yetu 4. Tanzania imekithiri ukiukwaji wa haki za binadamu , dhulma na kutekwa na serikali mhimili wa bunge pamoja mahakama. 5. Watanzania wapate fursa ...

Mahakama yamkuta na kesi ya kujibu Scopion atakiwa kujitetea Novemba 14

Image
Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemkuta na kesi ya kujibu mshtakiwa Salum Njwete maarufu kama Scorpion anaekabiliwa na kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi ambae aliingia kwenye vichwa vya habari baada ya kumtoboa mtu macho. Hatua hiyo inatokana na Hakimu Mkazi Flora Haule kusema kuwa amepitia ushahidi wa upande wa mashtaka na kujiridhisha na kuona mshtakiwa Njwete ana kesi ya kujibu. Hakimu Haule amesema kwa sababu hizo, Mshtakiwa anapaswa kutoa utetezi kwa njia atakazopenda kama kwa kiapo ama bila kiapo ambapo baada ya kueleza hayo, Mshtakiwa Njwete alisema kuwa atajitetea mwenyewe kwa njia ya kiapo lakini pia atakuwa na mashahidi wawili ambao walitumiwa kama Mashahidi wa upande wa mashtaka jambo ambalo Hakimu Haule amelikataa na kusema atafute mashahidi wengine au ajitetee mwenyewe. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Njwete anaetetewa na wakili Juma Nassoro anaidaiwa Septemba 6, 2016 saa 4 usiku maeneo ya Buguruni Ilala Dar es Salaam, aliiba cheni ya Silva yenye uzi...

Ongezeko la walaji wa nyama ya mbwa yazua taharuki China

Image
Serikali nchini China kupitia wizara yake ya Afya ya Wanyama na Ukaguzi imedai kuwa ongezeko la walaji wa nyama ya mbwa nchini humo kumepelekea ongezeko la kesi za watu kupotelewa na mbwa kuongezeka. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na shirika la Change.Org nchini China kwa mwaka zaidi ya mbwa milioni 20 huchinjwa kwa kitoweo ambapo inakadiliwa kuwa mbwa milioni 2 huchinjwa kwa mwezi ikiwa ni ongezeko la asilimia 15 ukilinganisha na mwaka 2015. Serikali ya China tayari imeanzisha msako wa kukagua leseni za bucha zinazotoa huduma ya kuuza nyama ya mbwa ili kubaini ukubwa wa ongezeko la bucha zinazofanya kazi bila kibali maalumu. Wiki iliyopita maafisa usalama nchini humo walikamata lori lenye mbwa 200 wakisafirishwa bila kibali maalumu na tayari mbwa hao wameshapata wenyewe. Taarifa hiyo imekuja baada ya maafisa usalama nchini humo kueleza kuwa kuna ongezeko la kesi za watu wakiripoti kila siku kupotelewa na mbwa majumbani kwao. Tayari wanaharakati nchini China wameungana na nc...

Zitto Kabwe ahamishiwa kituo kikuu cha Polisi Kanda Maalumu

Image
 Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameanza kuzungushwa katika vituo vya Polisi jijini Dar es Salaam. Zitto baada ya kuhojiwa katika Kituo cha Polisi cha Chang’ombe mkoani Temeke sasa amehamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu amesema baada ya Zitto kuhojiwa kuhusu aliyozungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za udiwani zilizofanyika Kijichi Jumapili Oktoba 29,2017 aliachiwa kwa dhamana. Shaibu amesema Zitto aliyewakilishwa na wanasheria Venance Msebo na Steven Mwakibolwa alidhaminiwa na watu wawili na alitakiwa kurudi kituoni hapo Jumatatu Novemba 6,2017. Hata hivyo, amesema alikamatwa tena. Akizungumzia kukamatwa kwa Zitto, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa  wanamshikilia kwa lugha za uchochezi. "Tunamshikilia kwa uchochezi na kutoa lugha zisizo na staha na yupo Central hapa,'' amesema Kamanda Mambosasa

Ni sawa kutumia mswaki mmoja na mpenzi wako?

Image
Jamani usiombe mapenzi yakakunogea utatamani ugandane na mpenzi wako kila mahala. Katika kona kona za mapenzi mapenzi leo nimekuta na hii kitu. Mara nyingi watu wanapokuwa katika mahusiano ya kimapenzi huwa wanaaminiana kupita kiasi hata kama hawakuwahi kuchunguza afya zao. Hali hii hupelekea wapenzi kuchangia vitu mbali mbali kama nyembe, mswaki,mkasi hata wengine hufikia hatua ya kuchangia pichuu! "ukivaa BOXER yangu na vaa KIBINI yako" Hapa leo nitahitaji tuongelea kitu kimoja. Mswaki,hivi ni sahihi wapenzi kuchangia mswaki? Na kiafya iko vipi, hakuna magojwa yoyote yanayoweka kutokea kwa kuchangia mswaki? Au matumaini yetu yako juu ya zile dawa za meno tupe Mtazamo wako.

Joti awajibu waliomsema kafunga ndoa na kiduku

Image
Jumamosi iliyopita ilikua harusi ya Mchekeshaji maarufu Tanzania Lucas Muhavile maarufu kama Joti ambapo gumzo lilikua pia nywele zake alizonyoa kwa staili ya kiduku na kuingia nacho Kanisani jambo ambalo lilifanya baadhi ya watu kuongea sana kwenye mitandao. Joti kwenye Exclusive Interview ambapo amewajibu waliomsema kuhusu kiduku chake, >>> “Sidhani kama kuna sheria au kuna maandiko yameandika kwamba ukinyoa hivi hutakiwi kufunga ndoa, hii sanasana iko kwenye maadili tu“ “Nilimuomba Padri na akanielewa na kuniambia wewe ni Msanii tunajua cha kufanya usisuke tu, fumua hizo nywele ziwe tu kawaida zibanebane vizuri”

Polepole:Nyalandu amejimaliza mwenyewe

Image
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amemponda aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akisema walishamweka pembeni kwa kuwa hakuwa mtu wa muhimu kwao. Akizungumza jana Jumatatu usiku katika kipindi cha Msemakweli kinachorushwa na Channel Ten, Polepole aliyekuwa akizungumzia mafanikio ya Rais John Magufuli kwa kipindi cha miaka miwili, alimtakia heri Nyalandu huku pia akisema amejimaliza mwenyewe. “Ameondoka mwanachama mmoja wa CCM leo (jana) amekwenda upinzani. Katiba yetu hii ya Jamhuri ya Muungano inasema kila mtu ana uhuru wa kujiunga na chama chochote. Tunaheshimu uamuzi wake, tunamkatia heri katika chama anakokwenda,” alisema Polepole. “Aliyeondoka leo ni ‘very insignificant’ yaani kwa Kiswahili hatujaona utofauti. Ndiyo maana sisi tumetoa maelekezo kwa Serikali kwamba, watu ambao hawakuweza kutukimbiza katika awamu ya tano kwenye maendeleo ya Taifa letu kwenye uongozi wa awamu ya tano wawekwe benchi kwanza. Sasa w...

Alikiba akataa kuitwa Mungu wa Bongo fleva msiniite hivo siwezi kuwa hivo

Image
Jinsi mashabiki wa soka wanavyochizika muda mwingine, ndivyo hivyo hata katika muziki. Kitu hiki kimemtokea shabiki mmoja wa Alikiba kitu kilichopelekea kumuita msanii huyo ‘Mungu wa Bongo Flava’. Hata hivyo kilikuwa ni kitu ambacho hakikumpendeza Alikiba, ndipo alipoamua kumjibu shabiki huyo ambaye anatumia jina la Kibasalu katika mtandao wa Instagram; Officialalikiba @kibasalu naomba msiniite hivyo siwezi kuwa wala siwezi kukubali imani yetu haturuhusu kujiita au kuitwa na mtu yoyote ule jina la MUUMBA. Comment hiyo ya Alikiba inakuja mara baada ya shabiki huyo kwenda kwenye moja ya picha za msanii huyo katika mtandao wa Instagram na kuandika, ‘Bongo flaver god’.

Miili 9 iliyokatwakatwa yapatikana kwenye nyumba Tokyo Japan

Image
Polisi nchini Japan wamemkamata mwanamume mmoja baada ya kupata viungo vya miili tisa katika nyumba yake iliyo Zama huko Tokyo. Polisi walipata vichwa viwili kwenye jokovu nje ya nyumba ya mshukiwa kwa jina Takahiro shiraishi, wakati wakichunguza kutoweka kwa mwanamke mmoja. Pia walipata viungo vya watu saba kwenye majokovu yaliyo ndani ya nyumba yake. Mtu huyo wa umri wa miaka 27 anashtakiwa kuwa ndiye alitupa miili hiyo. Polisi walikuwa wamepata miili ya wanawake 8 na mwanamume mmoja, mingine tayari ikiwa imeanza kuoza. "Niliwaua na nikaifanyia kazi miili yao ili kuficha ushahidi," shirika la habari la NHK lilimnukuu akisema. Jirani wake alisema kuwa alikuwa ameanza kuhisi harufu mbaya kutoka kwa nyumba yake tangu Bw. Shiraishi ahamie nyumba hiyo mwezi Agosti. Polisi walifanya ugunduzi huo walipokuwa wakimtafuta mwanamke wa umri wa miaka 23 ambaye amekuwa hajulikani aliko tangu tare 21 mwezi Oktoba. Wachunguzi waligundua kuwa Bw. Shiraishi amekuwa akiwasiliana na ...

Zitto aachiwa Polisi wamkamata tena

Image
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe, ameruhusiwa kwa kudhaminiwa na watu wawili hapa Kituo cha Polisi Chang'ombe, Temeke, Dar es salaam. Polisi wamemkamata tena baada ya kudhaminiwa kwa amri ya DCI, na muda huu anapelekwa kuhojiwa katika Kituo cha Polisi Kamata. Ado Shaibu Katibu - Kamati ya Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma ACT Wazalendo Oktoba 31, 2017

Profesa Jay atupa jiwe la gizani

Image
Mbunge wa Jimbo la Mikumi Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay ametoa ujumbe unaoonekana kama ushauri kwa vyama vya siasa huku ukilenga matukio ya hivi karibuni ya wanasiasa kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine. Katika Ukurasa wake wa mtandao wa Twitter Profesa Jay ameandika “Mkimaliza hiyo HOJA yenu Mfu ya UFISADI, leteni tuhuma za wote waliobaki huko na Muwatimue mapema msisubiri waondoke wenyewe... TUMEELEWANA”? Ujumbe huu wa Profesa Jay umekuja ikiwa ni chini ya saa 24 toka Mbunge wa Singida Kaskazini kupitia CCM, Lazaro Nyalandu ajiuzulu Ubunge pamoja na nyadhifa zingine ndani ya chama ikiwemo kujivua uanachama. Kwa upande mwingine ujumbe huo umechukuliwa kama jibu kwa Chama cha Mapinduzi ambacho kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole kilijibu suala la Nyalandu kuhama kwa hoja ya kuwa ni miongoni mwa wanachama wengi wasio waadilifu ambao wameamua kuondoka kabla ya Panga kuwafikia. Hata hivyo Profesa Jay amegoma kufafanua undani wa ujumbe h...

Kiongozi wa Katalonia aliyefutwa aenda Ubelgiji

Image
Rais wa Catalonia aliyefutwa Carles Puigdemont ameenda nchini Ubelgiji, wakili wake aliye chini humo anasema. Wakili huyo Paul Bekaert, hakuzungumzia ripoti kuwa Bw. Puigdemont anajiandaa kuomba kupewa hifadhi. Mwendesha mashtaka nchini Uhispania ametaka mashataka ya uasi kufunguliwa dhidi yake na viongozi wengine ya kura ya maoni iliyopogwa marufuku. Serikali ya Uhispania ilichukua udhibiti kamili wa Catalonia siku ya Jumatatu, kuchukua mahala pa viongozi waliofutwa. Ilifuta utawala wa eneo hilo na kuitisha uchaguguzi mpya baada ya Bw Puigdemont na serikali yake kujitangazia uhuru wiki iliyopita. Wakili huyo wa Ubelgiji Paul Bekaert alisema kuwa Bw. Puigdemont kwa sasa yuko mji mkuu wa Ubelgiji Brussels. Mbona Puigdemont akaenda Ubelgiji? Uhispania ilikuwa imekumbwa na mzozo wa kikatiba tangu kura ya maoni iliyopangwa na serikali ya Bw. Puigdemont, ilipoandaliwa tarehe mosi Oktoba kinyume na amri ya mahakama iliyoamua kuwa kura hiyo ilikuwa kinyume na katiba. Serikali ya Cta...

900 wasimamishwa shule kisa binti mmoja

Image
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, karibu wanafunzi 900 wa Shule ya Sekondari Kabale katika Manispaa ya Kabala nchini Uganda wamesimamishwa masomo kutokana na vurugu kubwa zilizoibuka shuleni hapo, chanzo kikielezwa ni kumgombea kimapenzi binti mmoja ambaye pia ni mwanafunzi shuleni hapo. Wanafunzi hao waliibua vurugu kubwa na kuanza kupigana mchana wa Ijumaa iliyopita shuleni hapo. Inaelezwa kuwa, mwanafunzi wa kidato cha sita aliomba kuwa na uhusiano na binti ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi mwingine wa kidato cha nne. Kutokana na kuvuja kwa taarifa hizo, makundi mawili ya wavulana hao yaliibua uhasama ulioishia kupigana. Ugomvi huo haukuishia kwa wanafunzi tu, waliharibu pia mali za shule na hata za majirani wanaoishi karibu na shule hiyo. Kutokana na hali hiyo, jeshi la Polisi lililazimika kuingilia kati kutuliza ghasia kwa kutumia mabomu ya machozi na silaha nyingine kutawanya wanafunzi hao. Kaimu Ofisa anayeshughulikia usalama wilayani Kabale, Kenneth Bir...

Jokate kuachana na mambo ya mziki

Image
MWANAMITINDO na msanii wa Bongo Fleva, Jokate Mwegelo amefunguka kuwa, ‘soon’ ataachana na muziki huo, bila kutaja sababu ya kufanya hivyo. Jokate aliiambia Full Shangwe kuwa, anajipanga kuachia wimbo mmoja wa mwisho kisha anaachana kabisa na Bongo Fleva. “Nafikiria kutoa wimbo moja wa mwisho, halafu baada ya hapo nitakuwa nimestaafu kufanya muziki, sina sababu ya msingi ila ni maamuzi yangu tu,” alisisitiza Jokate.

Aliyepanga kumuua Rais wa Urusi ajeruhiwa

Image
Amina Okuyeva na mumewe walipigana dhidi ya makundi yanayoiunga mkono Urusi Mwamamue moja kutoka Chechenia ambaye analaumiwa kwa kupanga kumuua rais wa Urusi Vladimir Putin amejeruhiwa na mke wake kuuliwa wakati wa shambulizi karibu na mji mkuu wa Ukrain Kiev. Adam Osmayev alijeruhiwa lakini anaweza kuishi baada ya gari alilokuwa akilitumia kumiminiwa risasi kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya ukrain. Wizara hiyo ilisema kuwa mke wake Osmaye, Amina Okuyev aliuawa wakati wa shambulizi katika kijiji cha Hlevaha. Mwaka 2012 maafisa nchini Urusi walisema kuwa Bw. Osmayev alikuwa sehemu ya njama ya wanamgambo kumuua Bwa Putin. Vyombo vya habari vya Urusi viliripoti wakati huo kuwa watu walipanga kutega mabamu kwenye barabara ya Kutuzovsky mjini Moscow, inayotumiwa na Bw Putin kila siku. Urusi baadaye iliitaka Ukrain kumsalimisha Bw. Osmayev lakini mamlaka nchini Urusi zikakataa kufanya hivyo, zikisema kuwa zilitaka kungoja hadi mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya kuamua kuhu...

Kinachoendelea polisi baada ya Zitto Kabwee kukamatwa

Image
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe, amekamatwa na polisi na kuhojiwa akituhumiwa kufanya makosa ya Uchochezi. Kwamba juzi, Oktoba 29, 2017 alipokuwa kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke alitoa maneno yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani. Maneno hayo ni yafuatayo: 1. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu mpaka siku hiyo.   2. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach. Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe.   Timu ya mawakili wa chama iko na ndugu Zitto katika mahojiano haya.   Ado Shaibu - Katibu wa Itikadi, Mwasiliano ya Umma na Uenezi ACT Wazalendo Oktoba 31, 2017 Dar es salaam

Makosa mawali anayotuhiwa kutenda Zitto Kabwe

Image
Upadates Kutoka Kituo cha Polisi Chang'ombe, mkoa wa kipolisi Temeke, Dar es salaam anakoshikiliwa Zitto Kabwe Kwamujibu wa taarifa kutoka kwenye kamati a sheria na katiba ya chama hicho, imeeleza kuwa Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe, amekamatwa na polisi na kuhojiwa akituhumiwa kufanya makosa ya Uchochezi. Kwamba juzi, Oktoba 29, 2017 alipokuwa kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke alitoa maneno yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani. Maneno hayo ni yafuatayo: 1. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu mpaka siku hiyo. 2. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach. Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe....

Meya wa jiji la Mwanza aachiwa huru Rais Magufuli awataka waache malumbano

Image
Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire jana aliachiwa na Polisi waliokuwa wakimshikilia kwa masaa kadhaa tangu asubuhi.    Akizungumza baada ya kuachiwa na polisi baada ya kuhojiwa   kwa saa saba jana, Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire,  alisema hatua hiyo inatokana   kutuhumiwa kutaka kuhatarisha msafara wa  Rais Dk.  John Magufuli wakati akiwasili Uwanja wa Ndege wa Mwanza. “Nikiwa uwanjani nilifuatwa na askari wawili ambao waliniambia nipo chini ya ulinzi. “Niliwauliza tatizo ni nini wao walinijibu wamepewa maelekezo kutoka juu kisha walinipeleka kituo kidogo cha polisi uwanjani na kuniweka hapo. “Baada ya rais kuondoka uwanjani nilichukuliwa na askari wengine watatu ambao walinipeleka kituo kikuu,” alisema. Alisema askari hao waliomfuata uwanjani walimchukua kwa gari dogo binafsi na alipofikishwa kituo kikuu cha polisi katika ofisi ya RCO (Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa), walimueleza kuwa wamea...

Rais Magufuli atangaza kiamaa kwa wakuu wa Mikoa

Image
Rais  Dk. John Magufuli amesema   mkuu wa mkoa yoyote atakayeshindwa kupeleka wawekezaji   kujenga viwanda katika mkoa wake hatamvumilia. Amewataka wakuu wote wa mikoa kuiga mfano wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, ambaye amekaribisha wawekezaji wanaojenga viwanda vipya. Agizo hilo alilitoa Mwanza jana alipokuwa akituhubia mkutano wa hadhara eneo la Nyakato wilayani Ilemela. Rais alisema viwanda si mali yake bali ni  mali ya wananchi ambao ndiyo walipa kodi. Alisema ingawa Tanzania ilikuwa na viwanda vingi, hivi  sasa Watanzania wamebaki hawapati majibu vilikwenda wapi  hali inayoifanya Serikali  iamue kufanya kazi ya kuvifufua vya zamani na kujenga vipya. Kabla ya kuhutubia mkutano huo Rais  alizindua kiwanda cha vinywaji baridi cha Sayona   kilichojengwa   Nyakato.  Leo anatarajiwa kuzindua viwanda vingine viwili. Alisema amefurahishwa na ahadi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela na kwamba ki...

Singida CCM wamjibu Nyalandu baada ya kutangaza kuhamia CHADEMA

Image
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida kimesema sababu zilizotolewa na aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu za kuacha ubunge hazina mashiko, isipokuwa kilichomsukuma kufukia uamuzi huo ni hasira za kukosa uwaziri. Katibu wa CCM mkoani Singida, Jamson Mhagama alisema jana Jumatatu Oktoba 30,2017 kuwa, “Kwa maono yake ameona siasa za nchi haziendi vizuri na kuamua kwenda kusaka siasa zitakazompendeza, tunamtakia kila la kheri. Ila tunamwonya kuwa asitarajie tena kupata ubunge kupitia Chadema anakolilia kwenda, CCM itashinda kwa kishindo katika uchaguzi mdogo ujao,” alisema. “Wananchi walimwamini Nyalandu katika vipindi vyote vinne kwa kumpa kura za kutosha za nafasi ya ubunge. Kupitia kura hizo, Nyalandu amesifika na kujulikana kila kona sasa ameamua kuwapa kisogo wakazi wa jimbo la Singida Kaskazini, jina lake linaenda kufutika na hatasikika tena,” amesema Mhagama. Katika hilo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida, William Mwang’imba...

Serikali yamjibu Zitto Kabwe. .. .. Yamp ONYO kali

Image
Na.Jacquiline Mrisho – MAELEZO. Serikali imetoa onyo kali kwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Mh. Zitto Kabwe juu ya taarifa za upotoshaji wa takwimu za Pato la Taifa alizozitoa hivi karibuni. Taarifa hizo za Mh. Zitto zimeripoti kuwa ukuaji wa Pato la Taifa kwa robo ya pili ya mwaka 2017 kuwa ni asilimia 5.7 badala ya asilimia 7.8. Kasi ya ukuaji ya asilimia 5.7 ilikuwa ni kwa robo ya kwanza ya Januari hadi Machi 2017. Onyo hilo limetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Bw. Daniel Masolwa Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa kutoka Ofisi ya Taifa za Takwimu (NBS),kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NBS,pamoja na  Mkurugenzi wa Sera na Tafiti za Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw.Johnson Nyella wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari. Masolwa alisema kuwa upotoshaji huo uliofanywa na Mh. Zitto ni wa makusudi na unalenga kuonesha kuwa juhudi znazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano hazina manufaa kwa Wananchi. “Napenda kukanusha kauli ya Mh. Zitto kuhusu taarifa zake...