Tundu Lissu:Walihangaika kunifungulia mashtaka waliposhindwa kunifunga wakaamua kunipigia risasi ila Mungu kaniponya

Tundu Lissu ameongea na Watanzania kuhusu mambo kadhaa.

Ameanza kwa kumshukuru Lazaro Nyalandu kwa Kuikimbia CCM na kuomba kujiunga CHADEMA. "Lazaro Nyalandu bado ana Mawazo ya Ujana".

Kingine alichozungumzia ni Uchaguzi mdogo wa Madiwani wa kata 43. Amesema watu wasiichague CCM. Amesema kuichagua CCM ni sawa na kukubali CCM wawndelee kufanya wanayoyafanya, nawaomba mfanye maamuzi Magumu.

Tukatae Mateso, tukatae Utawala wa Bomoabomoa, tukatae utawala wa kuokota maiti baharini kama samaki, tukatae utawala wa Kamatakamata, tuikatae CCM.

Nlipigwa risasi na walewale waliomfunga Diwani wa kata wa Siuyu bwana Gerald.

Walinifungulia mashitaka mara nyingi na waliposhindwa kunifunga wakaamua kunipiga risasi lakini Mungu kaniponya.

Kawaasa Wananchi wa Kata ya Siuyu Singida kuonyesha hisia zao. Amesema Watesi wetu wamelazimisha leo niongelee kitandani badala ya kuja kuongelea huko.

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara