Posts

Showing posts from November, 2017

Viongozi wawili wa Acacia wajiuzulu

Image
Dar es Salaam. Wakati utekelezaji wa makubalino baina ya Serikali na Barrick ukisubiriwa, Ofisa Mtendaji Mkuu na Ofisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya Acacia, wametangaza kujiuzulu kuanzia leo Alhamisi. Kwenye barua yake, Ofisa Mtendaji Mkuu, Brad Gordon amesema anataka kurudi nyumbani Australia kusimamia masuala ya familia yake wakati Ofisa Mkuu wa Fedha, Andrew Wray akisema amepata fursa nzuri zaidi sehemu nyingine. “Pamoja na uamuzi huo, wote wataendelea kuhudumu kwenye nafasi hizo wakati wakikabidhi majukumu ya ofisi kwa warithi wao,” imesema taarifa ya Acacia iliyotolewa leo Alhamisi asubuhi. Kuziba nafasi hizo, Bodi ya Wakurugenzi wa Acacia imemtangaza Peter Geleta kuchukua majukumu ya ofisa mtendaji mkuu baada ya Gordon na Jaco Maritz kusimamia masuala yote ya fedha za kampuni hiyo. Wote wawili walikuwa watendaji wa Acacia kwa muda mrefu. Geleta alikuwa mkuu wa oganaizesheni wakati Maritz alikuwa meneja mkuu wa idara ya fedha. “Licha ya majukumu ya uendeshaji...

Faida mbalimbali za Tangawizi katika mwili wa binadamu

Image
Hicho ni kiungo kinachotokana na mzizi wa mmea unaoitwa Tangawizi. Ni mmea unaofanana sana na binzari, ikiwa bado haijamenywa maganda yake. Pia, ni bidhaa inayopatikana nchi nzima kwa bei nafuu kabisa na kila mtu mwenye uwezo wowote wa kiuchumi, anaweza kununua aidha kwa kipande kimoja, fungu au hata kilo akipenda. Hivi karibuni akiwa mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, ambaye sasa ni mbunge wa Viti Maalum (CCM), aliendesha kampeni kubwa ya uzalishaji wa tangaweizi wilayani humo, ikiwa sehemu ya zao la biashara. Mmea huo unaweza kuonekana kama wa kawaida na watu kuutumia tu katika mtindo wa mazoea, lakini ni kiungo kinachotumiwa kama dawa. Pia, kiungo hicho kinaweza kutumika kikiwa ama kibichi au kimekaushwa na kutengenezwa katika mfumo wa unga. Faida zake Tangawizi ni kati ya mimea mingi yenye maajabu. Unaweza kutumika kama dawa na kutibu magonjwa zaidi ya 72 mwilini mwa mwanadamu. Ina faida zaidi hasa kwa wagonjwa walioathirika na maambukizi ya Ukimwi. Hivyo, kwa wale we...

Samata kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2017

Image
Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF imetaja orodha ya wachezaji 30, watakao wania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2017 huku jina la mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta anayecheza KRC Genk likiwemo katika  listi hiyo. Baadhi ya wachezaji waliyopo katika orodha ni pamoja na mshindi wa mwaka 2015, Pierre-Emerick Aubameyang, mshindi wa tatu mwaka 2016, Sadio Mane huku jina la mshindi wa mwaka jana, Riyad Mahrez raia wa Algeria likikosekana. Mbwana Samata (Tanzania & Genk), Vincent Aboubakar (Cameroon & Porto), Karim El Ahmadi (Morocco & Feyenoord), Christian Atsu (Ghana & Newcastle), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund), Eric Bailly (Cote d’Ivoire & Manchester United), Cedric Bakambu (DR Congo & Villareal), Keita Balde (Senegal & Monaco), Christian Bassogog (Cameroon & Henan Jianye), Yves Bissouma (Mali & Lille), Khalid Boutaib (Morocco & Yeni Malatyaspor), Yacine Brahimi (Algeria & Porto), Ess...

Mwamuzi Elly Sassi amjia juu manara

Image
Baada ya msemaji wa Simba Haji Manara jana kusema mwamuzi Elly Sassi aliwaonea kwenye mchezo dhidi ya watani wao wa jadi Yanga Novemba 28 mwamuzi huyo amejitokeza na kusema Haji Manara amekosa cha kuwaeleza Wanasimba. Elly Sassi amesema Haji Manara anatakiwa kujua sheria za soka kwanza ndio aongee vinginevyo aende TFF akapate mafunzo ya kuwa mwamuzi sio kuangalia tukio moja kisha kulitafsiri kiushabiki. “Nafikiri Haji Manara amekosa cha kuwaambia Wanasimba lakini matukio na maamuzi ya uwanjani siku ya mchezo hayana utata wowote kwa watu wanaojua sheria za soka ndio mana baada ya mchezo wakufunzi mbalimbali wa CAF walinipongeza”, amesema Elly Sassi. Mwamuzi huyo ambaye amejizolea sifa miaka ya hivi karibuni kutokana na uchezeshaji wake ameenda mbali zaidi na kutafsiri kisheria matukio ambayo Manara anahisi yalipaswa kuwa penalti. “Tukio la Yondani kisheria ni kweli alishika, lakini dhamira na namna ya tukio lilivyokuwa mkono haukuwa na mawasiliano na mpira na alik...

Jela miezi 6 kwa kuoa mke wa pili Pakistan

Image
Mahakama nchini Pakistan imemfunga mwanamume mmoja miezi sita jela ya kuoa mke wa pili bila ya idhini kutoka kwa mke wake. Mahakama hiyo ya mjini Lahore pia ilimuamrisha Shahzad Saqib, kulipa faini ya dola 1,900, na kukataa maoni yake kuwa dini ya kiislamu inamruhusu kuoa hadi wake wanne. Mke wa kwanza wa Sadiq Ayesha Bibi, alikuwa amefanikiwa kujitetea kuwa kuoa bila idhini yake ulikuwa ni ukiukaji wa sheria za familia nchini Pakistan. Wanaharakati wa masuala ya wanawake wabasema kuwa kesi hiyo ni pigo kwa ndoa za wake wengi. Mfasiri wa FBI afunga ndoa na mwajiri wa IS Pia walisema kuwa itawapa wanawake zaidi walio katika hali kama hizo motisha ya kupeleka kesi mahakamani. Nchini Pakistan, wanaume wanaotaka kuoa wanawake kadhaa hufanya hivyo baada ya miaka kadhaa na ni lazima wapate idhini kutoka kwa mke wa kwanza. Baraza la kiislamu nchini Pakistan ambalo hutoa ushauri wa serikali kuhusu masuala ya kiislamu, mara kwa mara limekosoa sheria za familia nchini humo. Sadiq ana h...

Watu 34 wahukumiwa kunyongwa

Image
Watu 34 wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, (Albino), ambapo matukio 67 ya ukatili dhidi ya albino yakiwa yameripotiwa. Takwimu hizo zimetolewa katika muendelezo wa mkakati wa kitaifa wa kupiga vita ukatili, mauaji na unyanyasaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi ambapo Wakili kutoka Ofisi Mkurugenzi wa Mashtaka, Beatrice Isembo, amesema, pamoja na adhabu za vifo, watuhumiwa 17 wamehukumiwa vifungo tofauti huku kesi nyingine zikiendelea. "Tumegundua mikoa ya kanda ya Ziwa ndiyo iliyoongoza kwa matukio ya aina hii  na yote ni kutokana na imani za kishiriki kama kutaka utajiri kwenye uvuvi, mazao nk." Mwanza inaongoza kwa kuwa na kesi za aina hii 15, na jumla ya matukio 67 yameripotiwa katika kipindi cha miaka 11" amesema Bi. Isembo. Kwa upande wake, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Ralph Meela, kutoka Makao Makuu ya jeshi la polisi Idara ya Upelelezi kitengo cha makosa dhidi ya binadamu na usalama barab...

Julio aanza majigambo

Image
KOCHA MKUU WA TIMU YA DODOMA FC YA DODOMA, JAMHURI KIHWELU ‘JULIO’,. KOCHA Mkuu wa timu ya Dodoma FC ya Dodoma, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, amesema matokeo mazuri ambayo timu yake inapata katika mechi za Ligi Daraja la Kwanza yanatokana na wao kujipanga na si kubebwa kama baadhi ya wadau wanavyosema. Akizungumza na gazeti hili jana, Julio, alisema kuwa anaamini kikosi chake kina nafasi ya kupanda daraja na kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao kwa sababu wamejipanga kuendelea kupambana ili watimize malengo waliyoyaweka. Beki na kocha huyo wa zamani wa Simba alisema pia ligi hiyo ni ngumu na ina changamoto mbalimbali huku akiweza wazi kukukutana na ushindani kwenye michezo yote wanayocheza. “Hakuna mechi rahisi, tunapambana katika kila mechi, hatubebwi, hata ukiangalia matokeo yetu, mechi nyingi tulizoshinda tumecheza ugenini, tutaendelea kupambana tutakaporudi kumalizika michezo ya nyumbani," alisema Julio. Baada ya juzi kupata ushindi wa mabao 2-1 ...

Omong hafukuzwi Simba

Image
KAIMU RAIS WA KLABU HIYO, SALIM ABDALLAH "TRY AGAIN. WAKATI mkataba wa Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, ukiwa umebakiza miezi minne kumalizika na hakuna mazungumzo yoyote ya kusaini mkataba mpya yaliyofanyika, Kaimu Rais wa klabu hiyo, Salim Abdallah "Try Again", ameibuka na kusema kuwa kocha huyo hafukuzwi. Minong'ono ya kutimuliwa kwa Omog imeendelea kwa kasi baada ya kutua kwa Mrundi Masoud Djuma Irambona, ambaye amerithi mikoba ya Jackson Mayanja aliyeamua kuachia ngazi na kurejea kwao Uganda kumaliza matatizo ya kifamilia. Akizungumza na Nipashe jana, Salim, alisema kuwa Omog bado ni kocha wa Simba na hakuna kikao chochote ambacho kimefanyika na kufikia uamuzi wa kumtimua kocha huyo raia wa Cameroon. Salim alisema kuwa mpaka sasa timu yao haijapoteza mchezo wowote kwenye ligi na anawaomba wote ambao wanafikiria Omog ataondoka kwenye klabu hiyo inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, kwa sasa waache kuwaombea "mabaya...

Lusinde amchana Nyalandu

Image
Kada Maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Jimbo la Mtera Mkoani Dodoma amewasihi Watanzania kumpuuza Mwanasiasa Lazaro Nyalandu ambaye juzi ametangaza kujivua nyadhifa zake zote katika CCM ikiwemo ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kwa kile alichodai Serikali kukigandamiza Chama na CCM kupoteza mwelekeo. Lusinde amesema Bw. Lazaro Nyalandu hakuwahi kunyimwa nafasi yoyote ya kutoa maoni yake ama dukuduku zake ndani ya chama wala bungeni na kwamba uamuzi huo unaashiria kuwa anatafuta kinga ya kutochukuliwa hatua kutokana na tuhuma nzito zinazomkabili. Kada huyo wa CCM amesema ana wasiwasi ndani ya Serikali wapo watendaji ama viongozi wasio waaminifu ambao watakuwa wamevujisha taarifa za hatua ambazo Serikali inatarajia kuzichukua dhidi kutokana na makosa makubwa aliyoyasababisha alipokuwa Waziri wa Maliasili na Utalii na alipokuwa Naibu Waziri.

Mwanamuziki huyu afariki Dunia

Image
Mwanamuziki Keith Wilder(65) amefariki dunia. Wider alikuwa akifanya vizuri na bendi yake ya Heatwave  kipindi cha miaka ya 70. Kupitia bendi yake hiyo wameshafanya hits song kama “Always and Forever,” “Boogie Nights” na “The Groove Line”, chanzo cha kifo chake kimetajwa kuwa ni matatizo ya kiafya. Taarifa ya kifo cha mkongwe huyo wa burudani imetolewa na binamu yake Billy Jones, ambaye ameeleza kuwa siku ya Jumapili marehemu alikuwa amelala na ndipo kifo kilipomkuta. Kupitia band yake wameshawahi kushiriki tuzo kubwa duniani za Grammys mara mbili ila hawakuwahi kushinda tuzo hizo.

Ajira za Afya zasitishwa

Image
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  Dar es Salaam. Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imesitisha ajira mpya za kada ya afya zilizoombwa kwa kipindi cha Agosti mwaka huu. Taarifa iliyotolewa Oktoba 31 na Tamisemi ikieleza kusitisha ajira hizo kwa walioitwa kazini. Taarifa hiyo iliwataarifu waajiri na waombaji wote wa nafasi za ajira za kada za afya kuwa imesitisha zoezi hilo kwa muda mfupi ili kukamilisha taratibu za ajira. “Tafadhali rejeeni tangazo letu lenye Kumb. Na CD. 162/355/01 la tarehe 30 Oktoba, 2017 lililowataarifu waombaji wa kazi wa nafasi mbalimbali za kada za afya walioomba kazi kuanzia 25/07 - 30/08/2017,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo. Taarifa hiyo imethibitishwa kutolewa na Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Zainabu Chaula ambaye aliliambia gazeti hili kuwa ni kweli wamesitisha kwa muda kwa sababu za kiufundi na halihusiani na madaktari wa Kenya. Hivi karibuni Waziri w...

Bashe:Mimi ni mbunge wa ndio mzee

Image
Mbunge wa Nzega Mjini(CCM) Hussein Bashe amefunguka na kusema wakati anaomba kura na Mhe. Rais Dkt. Magufuli mwaka 2015 alimwambia kiongozi huyo kuwa yeye hawezi kwenda bungeni na kuwa kati ya wale wabunge wa kusema 'Ndiyo' mzee. Bashe amesema hayo jana alipokuwa akiongea na wananchi wa jimbo la Nzega akiwaeleza mambo mbalimbali ambayo yamefanyika katika miaka miwili jimboni hapo toka alipochaguliwa kuwa Mbunge Oktoba 25, 2015.   "Mimi nikienda Bungeni nikisimama naposema nasema kweli kwa sababu kiapo cha CCM kinasema 'daima nitasema kweli unafiki kwangu mwiko'  "Huo ndio msimamo wangu na siku naomba kura na Mhe. Rais nilimwambia Rais jukwaani kwamba Mhe. Rais mimi siendi kuwa Mbunge wa ndio mzee bali mimi naenda kutimiza wajibu wangu na wajibu wangu ni kuisimamia, kuishauri na kuikosoa serikali" alisema Bashe Aidha Mbunge huyo alisema ataendelea kubaki na msimamo wake huo wa kuisimamia serikali labda mpaka wazee wa jimboni kwake wamshauri vinginevy...

Basi lagonga Treni na kujeruhi watu wawili

Image
Watu wawili wamejeruhiwa vibaya katika ajali ya basi la Nkondo lililokuwa likitokea Arusha kwenda Mwanza baada ya kugonga kichwa cha treni eneo la Karogho Relini katika Manispaa ya Shinyanga. Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo saa tatu usiku juzi barabara kuu iendayo Maganzo wakati basi hilo lenye namba za usajiri T 693 BUW aina ya Youtong mali ya Kampuni ya Nkondo likiendeshwa na dereva Emmanuel Warengo (34). Kamanda alisema katika ajali hiyo, watu wawili Ramadhani Juma (38) na Eva Brown (29) walijeruhiwa kwa kuumia kifuani na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa kupata matibabu.  Alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi kutochukua tahadhari wakati wa kuvuka barabara katika njia ya treni na alikimbia baada ya ajali hiyo na Polisi wanaendelea kumtafuta. Katika matukio mengine, Polisi imefanya oparesheni na kuwakamata watuhumiwa 29 wa makosa mbalimbali, kati ya hao saba kwa tukio la ukataji pa...

Watetezi wa haki ya wanyama walaani vifaranga kuteketezwa kwa moto

Image
Watetezi wa haki za wanyama wamelaani kuteketezwa vifaranga vya kuku 6,400 vilivyoingizwa nchini kinyume cha sheria. Vifaranga hivyo mali ya Mary Matia (23), vyenye thamani ya Sh12.5 milioni vilikamatwa mpakani Namanga vikitokea nchini Kenya. Kuteketezwa kwa vifaranga hivyo jana Jumanne Oktoba 31,2017 kumeibua mjadala ikielezwa kitendo hicho ni ukiukwaji wa sheria. Kazi ya kuviteketeza eneo la Namanga wilayani Longido ilifanyika ikishuhudiwa na maofisa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Wizara ya Mifugo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na vyombo vingine vya ulinzi na usalama. Akizungumza wakati wa kuviteketeza vifaranga hivyo, ofisa mfawidhi wa kituo cha udhibiti wa magonjwa ya mifugo Kanda ya Kaskazini, Obedi Nyasebwa amesema kazi hiyo imefanyika kwa kuzingatia Sheria ya Magonjwa ya Wanyama namba 17 ya mwaka 2003. Pia, amesema Serikali mwaka 2007 ilitoa tangazo kupiga marufuku kuingizwa nchini vifaranga vya kuku na mayai. Hata hivyo, watu mbalimbali wamehoji ulazima wa kuvi...

Papa Francis akiri kushikwa na usingizi wakati anapofanya maombi

Image
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis amekiri kwamba mara nyengine yeye hushikwa na usingizi wakati anapoomba. ''Wakati ninapoomba , mara nyengine mimi hushikwa na usingizi'', alisema katika kipindi kimoja cha kanisa hilo cha TV2000 kilichochapishwa katika mtandao wa You tube. ''Mtakatifu Theresa pia alikuwa akilala'', alisema kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80 kuhusu mtakatifu huyo wa karne ya 19. Lakini akasema kuwa kushikwa na usingizi wakati wa maombi huwa ''kunamfurahisha mungu na kwamba Wakristo walitakiwa kuhisi kama watoto wanaolalia mkono wa baba yao''. Ripoti zinasema kuwa papa Francis hulala mwendo wa saa tatu na kuamka saa kumi alfajiri kila asubuhi. Raia huyo wa Argentina amekuwa kiongozi wa kanisa katoliki tangu 2013 na amekuwa na ratiba ilio na mambo mengi ya ziara za kigeni na mikutano ya kuonekana hadharani. Amekuwa maarufu kwa baadhi ya mabadiliko na uwazi katika uongozi wake hususan katika ut...

Dr. Mashinji aamua kufunguka

Image
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Vicent Mashinji‏ ametupa jiwe gizani na kudai kwamba kitendo cha dola kumkamata mtu kwa tuhuma za uchochezi ni udhaifu wa serikali katika kujibu hoja. Dr. Mashinji amesema kwamba siasa zenye msamiati wa  uchochezi huwa hazipo hivyo kwani wadhaifu huwa ndiyo wanaotumia mabavu na siyo hoja. Kupitia ukurasa wake wa Twitter Dkt Mashinji ameandika "Najenga hoja, unasema mi mchochezi. Kweli umekosa ushawishi jitafakari upya, siasa za sasa msamiati wa uchochezi haupo. Ni hoja kwa hoja!" Hivi karibuni viongozi mbalimbali wa upinzani wamekuwa wakikamatwa na jeshi la polisi mara kwa mara kwa tuhuma za uchochezi

Nyalandu afukuzwa uanachama wa CCM

Image
Ofisi ya Spika wa Bunge ingependa kuwaarifu Watanzania wote kwamba mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini (CCM) Ndugu Lazaro Nyalandu ambayo amekuwa akiarifu kwamba amemwandikia Mheshimiwa Spika kumtaarifu kujiuzulu kwake. Hata hivyo, Mhedhimiwa Spika amepokea barua toka kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ya tarehe 30 Oktoba, 2017 akimuarifu kwamba kwa muda sasa Chama hicho kilishaanza kumchukulia hatua za kiudhibiti na kinidhamu dhidi ya vitendo na kauli zake zisizoridhisha kinyume na misingi, falsafa na itikadi ya Chama cha Mapinduzi. Hivyo, Chama cha Mapinduzi kuanzia tarehe ya barua yao kimemjulisha Mheeshimiwa Spika kuwa Ndugu Lazaro Nyalandu amepoteza sifa za Uanachama wa Chama cha Mapinduzi, na hivyo kupoteza nafasi zote za uongozi wa ndani wa Chama hicho na Ubunge kwa mujibu wa Ibara ya 13 ya Chama hicho. Mheshimiwa Spika, angependa kuwaarifu Watanzania kwamba kwa barua hiyo toka mamlaka halali ndani ya Chama cha Mapinduzi a...

Waziri mkuu awafunda watanzania waishio Canada

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waishio Canada wadumishe mshikamano wao na wawe na uzalendo kwa Taifa lao. Ametoa kauli hiyo Jumanne, Oktoba 31, 2017 wakati akizungumza na Watanzania waishio Toronto, Canada. Waziri Mkuu ambaye yuko Canada kwa ziara ya kikazi, alisema kila Mtanzania anapaswa ahubiri utaifa wake. “Wakati wote ringia nchi yako, unapotakiwa kuisemea nchi yako, isemee vizuri kama ambavyo wengine wanasemea vizuri nchi zao licha ya matatizo waliyonayo.” Alisema Serikali inawasisitiza wananchi wake hasa waishio nje ya nchi, wawe wazalendo na washirikiane kuhakikisha wanazitumia fursa za kimaendeleo vizuri kwa ajili ya manufaa ya nchi yao. Awali, Balozi wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Nzoka, alitumia fursa hiyo kuwasihi Watanzania hao wazingatie sheria za nchi wanayoishi. “Wote sisi tunawatambua kama mabalozi katika nafasi zenu hapa Canada. Tunawashauri muwe raia wema, na muishi kwa kufuata sheria na taratibu za nchi hii na msisahau...

MAGAZETI YA LEO 2/11/2017

Image

Mke wa mtu na mchepuko wake wakutwa wamekufa kwenye gari wakiwa wanafanya mapenzi

Image
Mwili wa mwanamke mmoja aliyeripotiwa kuwa ni mke wa mtu mwenye watoto wanne umekutwa kwenye taxi mjini Lagos, nchini Nigeria ukiwa juu ya kifua cha mwanaume ambaye nae alikuwa ameshakufa. Wote wawili wakiwa wamelaliana wakishiriki tendo la ndoa. Gari lililokutwa kwenye eneo la tukio Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililotokea jumapili ya wikiendi iliyopita wamesema walikuta gari dogo (Taxi) ikiwa imepaki na ndani kukiwa na watu waliokuwa uchi wakiwa wamelaliana ndipo wakaamua kuchukua uamuzi wa kufungua milango. Shuhuda mmoja alikiri wazi kumfahamu mama huyo na kudai kuwa ameolewa na ana watoto wanne huku akishindwa kumtambua mwanamme aliyekuwa naye. Baadhi ya maelezo ya mashuhuda kupitia mitandao ya kijamii wamesema walikuta gari na AC ikiwa imewashwa. Hata hivyo hakuna taarifa rasmi kutoka jeshi la polisi nchini humo kuhusu tukio hilo la kusikitisha.Pitia baadhi ya tweets za mashuhuda wa tukio hilo.

Halima Mdee amuunga mkono Zitto Kabwe

Image
Baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kuomba kuunganisha nguvu ya pamoja na CHADEMA ili kufanikisha kuing'oa CCM kwenye chaguzi ndogo za madiwani, Halima Mdee amefunguka na kusema kwamba hatoshangaa chama chake kushirikiana na ACT Wazalendo. Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe kupitia CHADEMA ameyasema hayo alipokuwa akiongea na mwandishi wa East Africa Television, na kueleza kwamba wao kama wanasiasa wanaangalia ni namna gani wanaweza kufikia lengo kwa pamoja, hivyo sio mbaya kama wataungana na ACT Wazalendo kufanikisha mambo ambayo wao pia wanayapigania. Halima Mdee ameendelea kwa kusema kwamba sasa hivi ana imani na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye alifukuzwa kwenye chama hicho wakimuita msaliti, na kwamba kiongozi huyo sasa anarudi kwenye mstari ambao unamfaa.

Lazaro Nyalandu awashukuru Watanzania

Image
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu amefunguka na kuwashukuru Watanzania mbalimbali ambao wamekuwa na yeye katika maamuzi magumu aliyofanya kuachana na CCM pamoja na kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kupitia chama hicho. Nyalandu amesema kuwa hoja zilizopo mbele kwa sasa ni kubwa kuliko mtu mmoja mmoja na zinalenga kuleta utashi kwa kila Mtanzania kutafakari na kushiriki kikamilifu katika safari ya kuendeleza nchi katika Demokrasia, uchumi na kijamii. "Nachukua nafasi hii kumshukuru kila mmoja wetu ayenitumia salaam na kuunga mkono hatua niliyochukua. Hoja zilizombele yetu ni kubwa kuliko mtu binafsi mmoja mmoja, na zinalenga kuhuisha utashi wa kila Mtanzania kutafakari na kushiriki kikamilifu safari ya kuiendeleza nchi yetu Kidemokrasia, kiuchumi, na kijamii. Ni maombi yangu kuwa, ujasiri ukaondoe roho ya woga, upendo uondoe chuki, nia njema iondoe kuoneana, na kweli ituweke huru na iondoe roho ya kusingiziana kunakoleta kuumizana na sintofahamu ya hali ya juu...

Yanga kusepa na wachezaji 22

Image
Jumla ya wachezaji 22 na viongozi wa Benchi la Ufundi la Yanga kesho saa 11:30 alfajili wanatarajia kusafiri kwa basi kuelekea Singida kwa ajili ya kupambana na Singida United. Timu hizo, zinatarajiwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Namfua huko Singida katika mechi ya LigI Kuu Bara. Yanga inatarajiwa kusafiri bila ya nyota wake muhimu wanne, Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Thabani Kamusoko ambao majeruhi na Juma Abdul anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano. Timu hiyo, ilifanya mazoezi yake ya mwisho saa 3:00 asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mechi na Singida inayofundishwa na kocha wa zamani wa timu hiyo Mholanzi, Hans Pluijm. Katika mazoezi hayo, kocha wa timu hiyo  alionekana akiwapa mbinu mbalimbali za aina ya uchezaji ndani ya uwanja ili kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mechi hiyo.

Mwanadada atembezwa uchi mbele ya mamia ya wanakijiji

Image
Mwanadada mmoja katika mji wa Dera Ismail Khan nchini Pakistan ametembezwa uchi wa mnyama mbele ya mamia ya wanakijiji ili kufidia adhabu ya kaka yake aliyezini na msichana mdogo kiumri mwaka 2015. Taarifa kutoka kwenye gazeti la Tribune la nchini humo zinaeleza kuwa kaka wa msichana huyo aliyetembezwa akiwa uchi, alifanya mapenzi na binti wa familia nyingine hivyo baraza la kijiji liliamuru kaka huyo alipe kiasi cha rupia 150,000 za Pakistan sawa na Tsh milioni 2.2 mwaka jana ili kuyamaliza matatizo hayo kifamilia. Hata hivyo familia ya Mwanaume huyo mzinifu aliyetambulika kwa jina la Sajjad ilishindwa kutoa fedha hizo ndipo baraza hilo la kijiji lijulikanalo kama (Panchayati) lilipotoa hukumu hiyo ya kumtembeza dada wa Sajjad uchi wa mnyama mbele ya wanakijiji ili liwe funzo kwa familia nyingine. Tayari polisi nchini Pakistan wametangaza kuwakamata watu saba kufuatia tukio hilo la udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia, wengi wa waliokamatwa ni viongozi wa baraza la kijiji wal...

Malima afutiwa Kesi

Image
Siku sita baada ya Adam Malima kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mahakama imemfutia kesi ya shambulio iliyokuwa ikimkabili. Rais John Magufuli, Alhamisi Oktoba 26,2017 alifanya uteuzi mbalimbali ukiwemo wa wakuu wa mikoa. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatano Novemba 1,2017 imeifuta kesi dhidi ya Malima na mwenzake. Malima ambaye amesharipoti mkoani Mara hakuwepo mahakamani wakati uamuzi huo ukitolewa. Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage ameifuta kesi hiyo na kuwaachia huru washtakiwa baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kuomba ifutwe. Chini ya kifungu cha 91 (1) cha Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, Mutalemwa ameomba shauri lifutwe kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendeleza mashtaka dhidi ya washtakiwa. Baada ya ombi hilo kuwasilishwa, Hakimu Mwijage alimuhoji Mutalemwa iwapo kuna sababu ya kuifuta kesi hiyo na kama hana hataifuta. Wakili Mutalemwa alisoma kifungu hicho akisema kinampa mamlaka DPP kuiondoa kesi mahakamani waka...

Hakimu:Wema Sepetu hakufanyiwa upekuzi kwenye Maungo yake

Image
November 1, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea kielelezo cha hati ya ukamataji mali nyumbani kwa Wema Sepetu anayekabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya. Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya wakili wa serikali, Elizabeth Mkunde kusema kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi. Katika uamuzi wake, Hakimu Simba amesema amepitia hoja zote za upande wa mashtaka na utetezi kuhusu hoja za kupokelewa ama kutopokelewa kielelezo hicho, ambapo ameona akipokee. “Mahakama inatupilia mbali pingamizi la utetezi la kutaka kielelezo kisipokelewe, hivyo nimekubaliana na hoja za upande wa mashtaka na kielelezo kinapokelewa,” Hakimu Simba amesema sababu za kupokea kielelezo hicho ni kwamba Wema hakufanyiwa upekuzi kwenye maungo ya mwili wake bali ni nyumba yake, hivyo haina tatizo kama ilipekuliwa na askari wakiume. ” Kama upekuzi ungeusu maungo ya mwili wake basi kungekuwa na tatizo, lakini umefanyika nyumbani kwake,”. Ba...

Kesi ya Mpemba wa Magufuli kupelekwa Mahakama ya Mafisadi

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo November 1, 2017 imeelezwa kuwa jalada la kesi ya kujihusisha na biashara haramu ya meno ya Tembo ya Tsh. Milioni 785 inayomkabili Mfanyabiashara Yusuf Ali maarufu kama ‘Mpemba wa Magufuli’ linaandaliwa kupelekwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kwenye ‘Mahakama ya Mafisadi’ Haya yameelezwa na Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo ulishakamilika na kinachofanyika sasa ni jalada la kesi hiyo kuandaliwa ili liende Mahakama ya Mafisadi. Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi November 15, 2017 ambapo katika kesi hiyo mbali ya Mpemba, Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Charles Mrutu, mkazi wa Mlimba, Morogoro, Benedict Kungwa, mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima, mkazi wa Mbezi, Ahmed Nyagongo, dereva na Pius Kulagwa. Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno ...

Taarifa ya Spika Ndugai kuhusu kujiuzulu mh. Nyalandu

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema amepokea barua ya Katibu Mkuu CCM ikimuarifu kuwa walishaanza kumchukulia hatua Nyalandu kutokana na kauli na vitendo vyake. Ambapo CCM imeeleza kuwa Oktoba 30 walimuandikia Spika barua kuwa, Nyalandu amepoteza sifa za uanachama wake na kwamba wamemvua nafasi zote za uongozi, hata hivyo Spika amesema kuwa hajapokea barua ya kujiuzulu kwa mbunge huyo.