Wayne Rooney Ateswa na Upara

Mshambuliaji wa Everton, Wyne Rooney ameingia na hofu ya kukosa nywele baada ya upara kuanza kuonekana.

Mchezaji huyo alionekana kwenye picha aliyotuma hivi karibuni mtandaoni ikimuonyesha nywele zake zikiwa zimeanza kupukutika.

Rooney analazimika kutumia takribani Pauni 30,000 kwa ajili ya kuweka sawa nywele zake.

Rooney amekumbwa na hali ya kuanza kuota kipara tangu akiwa bado kijana ambapo hivi sasa ana miaka 32.

Hivi karibuni mchezaji huyo alikutwa na mashtaka ya kuendesha akiwa amelewa, jambo lililosababisha kuhukumiwa kutoendesha magari yake kwa miaka miwili huku akilimwa na faini.

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara