Watahiniwa 385, 938 kidato cha nne kuanza mitihani kesho

Jumla ya watahiniwa 385,938 wamesajiliwa kwa ajili ya kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu ambapo mitihani hiyo inatarajiwa kuanza rasmi kesho kwa nchini nzima.

Akitoa taarifa za mitihani hiyo Katibu Mtendaji wa Baraza la  mitihani la taifa Dk Charles Msonde amesema kati ya watahiniwa 385,938,watahiniwa wa shule ni 323,513 na watahiniwa wa kujitegemea ni 62,425 akaongeza kuwa taratibu za mitihani lazima zifuatwe.

Aidha Katibu huyo amesisitiza kuwa bado kanuni na sheria za mitihani haziruhusu watu wasiohusika na mitihani kufika katika maeneo ya shule kwani watahiniwa wanahitaji utulivu mkubwa na hivyo jamii na watu wote waelewe hivyo.

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara