Vimewasili vifaa vya upanuzi wa bandari ya Dar es salam

Akizungumza na waandishi wa habari  katika eneo ambalo meli zilizobeba vifaa hivyo imetia nanga meneja wa bandari ya Dar es Salaam Bw. Fred Liundi amesema  mradi huo ukiimalika utakuwa na uwezo wa kuhudumia  meli kubwa kutoka urefu wa  wa sasa wa meta 243 hadi kufikia  urefu wa meta 320.

Hata hivyo meneja huyo amewatoa wasiwasi watumiaji wa bandari hiyo kuwa ujenzi ukianza huduma hazitasimama.

Bi.Anastazia  Saled ni msimamizi wa mradi huo ambaye anasema wamejipanga vyema kuhakisha kuwa ujenzi unafanyika katika viwango vinavyokubalika.

Upanuzi wa bandari hiyo unafanywa na kampuni kutoka china ya China Harbour  Enginering  CO ambapo mbali na kuongeza kina cha Bandari pia watajenga gati mpya  kwa  ajili ya kususha magari.

.

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara