Upinzani Kenya wataka uchaguzi ufutwe tena

Mmoja wa viongozi wa Nasa Musalia Mudavadi ameshutumu hatua ya tume ya uchaguzi kuahirisha uchaguzi majimbo manne magharibi mwa Kenya na kusema utafanyika kesho Jumamosi.

Bw Mudavadi ametoa wito kwa tume ya uchaguzi kufuta uchaguzi huo.

Amewashutumu polisi akisema wamekuwa wakitumia nguvu kupita kiasi kukabiliana na wakazi katika maeneo yanayoaminika kuwa ngome ya upinzani.

"Serikali hii haijafurahi kwamba watu wameikataa, inatumia nguvu kuwakabili wapinzani wake," amesema.

Hata hivyo Bw Odinga amewaambia wafuasi wake Kibera, Nairobi kwamba atatangaza hatua ya kuchukua Jumatatu.

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara