Shiza Kichuya afikia rekodi hii
Shiza Ramadhani Kichuya amefunga goli lake la tatu mfululizo dhidi ya Yanga kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara tangu asajiliwe na Simba msimu uliopita akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Leo October 28, 2017 Kichuya amefunga goli la Simba kwenye sare ya 1-1 dhidi ya Yanga. Kichuya alifunga bao hilo likiwa ni la kuongoza dakika ya 58 kipindi cha pili lakini halikudumu baada ya Obrey Chirwa kuisawazishia Yanga dakika ya 60.
October 1, 2016 Kichuya aliifunga Yanga kwa mara ya kwanza akiwa Simba bao lake likiwa ni la kusawazisha wakati timu hizo zilipotoka sare ya kufungana 1-1 kwenye uwanja wa taifa.
February 25, 2017 Kichuya akaifunga tena Yanga kwa mara ya pili mfululizo kwenye mechi za ligi Simba ilipopata ushindi wa magoli 2-1 kwenye uwanja wa taifa.
October 28, 2017, Kichuya ameweka rekodi ya kuifunga Yanga kwa mara ya tatu mfululizo kwenye mechi za VPL mechi iliyochezwa uwanja wa Uhuru, Dar.
Mechi ambazo Kichuya ameifunga Yanga mfululizo
October 1, 2016 Simba 1-1 YangaFebruary 25, 2017 Simba 2-1 YangaOctober 28, 2017 Yanga 1-1 Simba
Kichuya amefikia rekodi ya Amis Tambwe
Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe aliwahi kuifunga Simba mara tatu mfululizo tangu alipojiunga na Yanga baada ya kutemwa Simba.
September 26, 2015 Tambwe aliifunga Simba kwa mara ya kwanza akiwa mchezaji wa Yanga wakati Yanga iliposhinda 2-0 kwenye mchezo wa ligi.
Alifunga kwa mara ya pili kwenye ushindi mwingine wa Yanga 2-0 Simba September 20, 2016 bao lake la tatu mfululizo dhidi ya Simba alilifunga October 1, 2017 wakati timu hizo zilipotoka sare ya kufungana 1-1.
Rekodi ya Amis Tambwe ya magoli matatu mfululizo vs Simba
September 26, 2015 Simba 0-2 YangaSeptember 20, 2016 Yanga 2-0 SimbaOctober 1, 2017 Yanga 1-1 Simba
Comments
Post a Comment