Shehena ya vifaa ya uboreshaji ya bandari ya Dar vyawasili
Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo ambalo meli zilizobeba vifaa hivyo imetia nanga meneja wa bandari ya Dar es Salaam Bw. Fred Liundi amesema mradi huo ukiimalika utakuwa na uwezo wa kuhudumia meli kubwa kutoka urefu wa wa sasa wa meta 243 hadi kufikia urefu wa meta 320.
Hata hivyo meneja huyo amewatoa wasiwasi watumiaji wa bandari hiyo kuwa ujenzi ukianza huduma hazitasimama.
Bi.Anastazia Saled ni msimamizi wa mradi huo ambaye anasema wamejipanga vyema kuhakisha kuwa ujenzi unafanyika katika viwango vinavyokubalika.
Upanuzi wa bandari hiyo unafanywa na kampuni kutoka china ya China Harbour Enginering CO ambapo mbali na kuongeza kina cha Bandari pia watajenga gati mpya kwa ajili ya kususha magari.
Comments
Post a Comment