Shambulizi lingine nchini Somalia laua 6
Watu 6 wakiwemo wanawake wawili wamefariki katika shambulizi lililolenga gari moja la uchukuzi wa umma katika mji wa Deniga katika mkoa wa Shabele kusini mwa Somalia.
Shambulizi hilo limetelekezwa na bomu la kutegwa ardhini ambalo lililipuka wakati gari hilo likipita. Tukio hilo limetokea katika barabara inayounganisha mjini Shabele ya kaskazini na Shabele na Kaskazini.
Taarifa hiyo ilitolewa na naiba wa gavana wa eneo hilo Ali Nur.
Ali Nur amesema kuwa wanamgambo wa al Shabaab wanashambulia kwa kuvizia magari ya jeshi la serikali na jeshi la Umoja wa Afrika nchini humo.
Hakuna kundi lolote ambalo limejinasibu kuhusika na shambulizi hilo.
Ikumbukwe kuwa shambulizi la kigaidi Oktoba mjini Mogadishu lilisababisha vifo vya watu zaidi ya 300 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 220.
Comments
Post a Comment