Shambulizi la kujitoa Muhanga Nigeria laua 13

Watu 13 wafariki katika shambulizi la kujio muhanga  lililotekelezwa Kaskazini mwa Nigeria

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na msimamizi wa kitengo cha kuchunga usalama Damian Chukwu ni kwamba watu 13 wameuawa na wengine 18 wamejeruhiwa katika shaömbulizi la kujitoa muhanga.

Shambulizi hilo la kujitoa muhanga limetekelezwa katika eneo la Borno Kaskazini mwa Nigeria.

Taarifa zimesemakuwa shambulizi moja limetekelezwa Maiduguri huku mashambulizi mengine mawili katika eneo la Muna Dalti.

Licha ya kuwa hakuna kundi lolote lililojinasibu kuhusika na mashambulizi hayo, kundi la Boko Haram linakisiwa kuhusika na mashambulizi hayo.

Kundi la Boko Haram limeanza kushambulia vikosi vya serikali na raia tangu mwaka 2009 baada ya kifo cha kiongozi wao.

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara