Samatta kuibuka na mabao Ubelgiji

KRC Genk imeendeleza ushindi nchini Ubelgiji baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Club Brugge.

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ameendelea kuonyesha uwezo wake wa kufunga baada ya kushindilia msumari wa mwisho.

Samatta amefunga bao la pili katika dakika ya 90 baada ya Ruslan Malinovsky kuwa amefunga bao la kwanza katika dakika ya 43.

Samatta angeweza kufunga bao katika kipindi cha kwanza lakini mpira alioupiga ulipaa juu ya lango.

Muda mwingi Mtanzania huyo alikuwa mwiba mbele ya mabeki wa Club Brugge lakini walikuwa makini kuhakikisha hafungi.

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara