Roboti aliepewa jina la Sophia apewa uraia nchini Saudi Arabia. kwa mujibu wa mtandao wa turkey imeeleza kuwa ni kwa mara ya kwanza ulimwenguni roboti kupewa uraia.
Wengi wetu tukila ndizi mbivu huwa tunatupa maganda ya ndizi, lakini ukweli ni kwamba maganda ya ndizi yana faida lukuki kama ifutavyo; 1.Husaidia kung'arisha meno. Unachotakiwa kufanya ni; Chukua sehemu ya ndani ya ganda la ndizi na kisha sugulia kwenye meno itasaidia kuyafanya meno yako kuwa meupe. 2.Husaidia kuondoa vipele vya mbu na wadudu. Unachotakiwa kufanya ni; Tumia ganda la ndizi kwa kusugulia sehemu uliyoumwa na mdudu au mbu ili kuondoa maumivu na wekundu. 3. Huondoa mikunjo usoni ( wrinkles) Unachotakiwa kufanya ni; Changanya ute wa yai na nyuzi nyuzi za ndani ya ganda la ndizi kisha paka usoni kwa dakika 20, ili kupoteza mikunjo. Hizo ni faida chache kati nyingi ya kutumia ganda la ndizi.
Kurudisha nguvu za kiume Makala hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu na si vinginevyo au kama elimu kwa wanandoa watarajiwa. Muogope Mungu uzinzi ni dhambi kubwa sana. Katika kilele cha juu kabisa cha furaha katika ndoa, kama inavyojulikana, ni sherehe inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa. Ingawa, ili furaha hiyo ipatikane ni lazima tendo hilo liwe limefanyika katika hali ya afya kwa wanandoa wote wawili. Nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’. Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine. Inaweza kuwa ni hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha. Pamoja na hayo yote, elimu mhimu ambayo mwanaume anatakiwa kuwa nayo, ni kuwa nguvu za kiume hazipatikani kwa kutumia madawa ya kemikali au mahala pengine; bali zinat...
Jina kamili : Ernesto Guevara Kazi : Daktari, mwanamapinduzi wa kijamaa (marxist) Uraia : Argentina Kuzaliwa : June 14 1928 Kufariki : October 9, 1967 ,Bolivia milima ya La heguera Chanzo cha kifo : kuuwawa kwa kupigwa risasi Kama kijana msomi wa shahada ya udaktari, che Guevara alisafiri nchi nyingi sana huko bara la Amerika ya kusini na rafiki yake, akawa ni mtu mwenye uchungu mkubwa kuona maisha ya dhiki,njaa, magonjwa nchi za America ya kusini, akawa na mwamko mkubwa kubadili hali ile kwa kuwa aliamini ya kuwa mfumo wa ubepari ndio chanzo kikubwa kilichokuwa kinaitafuna Latin America. Miaka ya 50 akiwa anasoma udaktari huko Mexico Che Guevara alikutana na Fidel Castro na Raul Castro ambapo watatu hao walipanga mapinduzi ya kumg’oa raisi wa Cuba wakati huo Fulgencio batista ambaye alikuwa na huhusiano wa kimaslahi na America, Che akapata nguvu na uaminifu mkubwa kutoka kwa Fedel Castro na kupandishwa kuwa kiongozi wa wanamgambo (gueri...
Comments
Post a Comment