Odinga asema anajianda kwa uchaguzi mwingine

Kiongozi wa Muungano wa Upinzani, Nasa, nchini Kenya, Raila Odinga, amepuuzia uchaguzi wa marudio wa Urais uliofanyika jana nchini humo na kudai kwamba haukuwa wa halali, hivyo anajiandaa kwa uchaguzi mwingine.

Odinga amesema, uchaguzi huo haukuwakilisha Wakenya walio wengi hivyo yeye anajiandaa kwa uchaguzi mwingine utakaofanyika baada ya siku 90.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kufanyika kwa uchaguzi huo wa marudio, Odinga amesema kwamba uchaguzi huo mwingine utafanyika hata kama malalamiko yao hayatashughulikiwa na Tume ya Uchaguzi IEBC.

Odinga amesisitiza kwamba, muungano wa upinzani, hauutambui uchaguzi huo wa marudio kufuatia kuvurugika katika baadhi ya maeneo nchini humo.

Odinga aliamua kujitoa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo wa marudio uliofanyika hana Oktoba 26 baada ya ule wa Agosti 08 kutenguliwa na mahakama kwa madai kwamba ulikuwa na dosari nyingi

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara