Nape Nnauye amtabiria ushindi Kenyatta

 Mbunge wa Mtama, Nape Moses Nnauye amefunguka na kumtabiria ushindi mgombea Urais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kusema kuwa atashinda uchaguzi huo ambao unafanyika leo Alhamisi Oktoba 26, 2017 na kusema Uhuru ndiye anayestahili kuongoza nchi hiyo.

 Nape Nnauye amedai kuwa Uhuru Kenyatta anastahili kuwa Rais wa Kenya kwa sababu yeye ni mwana demokrasia wa kweli hivyo anaamini raia wa Kenya watampa kura nyingi za kutosha na kumpuuza mpinzani wake Raila Odinga.

"Unastahili kuwa Rais wa Kenya. Mwana demokrasia wa kweli. Naamini ndugu zangu wa Kenya watakuchagua kwa kishindo kesho na kumpuuza kibaraka" ameaandika Nape Nnauye kupitia mtandao wake wa twitter.


Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara