Mmoja wa pacha waliotenganishwa India afungua macho

Haki miliki ya pichaAIIMSImage captionMmoja wa pacha waliotenganishwa India afungua macho

Mmoja wa watoto pacha ambao walizaliwa wakiwa wameshikana kwenye vichwa amefungua macho yake siku nne baada ya upasuaji wa kuwatenganisha nchini India.

Jaga, mwenye umri wa miaka miwili aliweza kuitikia ishara ndogo kama kusongesha mikono yake.

Ngugu yake, Kalia hata hivyo bado hajapata fahamu

Watoto hao walizaliwa wakiwa wanatumia kwa pamoja mishiba na nyama za ubongo na upasuaji uliochukua saa 16 uliwatenganisha.

Watoto hao wote wako hali nzuri na madaktari wameridhishwa na vile wanavyoendelea hadi sasa, Professor Deepak Gupta, ambaye alishiriki katika upasuaji huo aliiambia BBC.

Haki miliki ya pichaAIIMSImage captionMadaktari wanasema pacha hao wako hali nzuriHaki miliki ya pichaAIIMSImage captionPacha hao kabla ya upasuaji wa kuwatenganisha

Pacha hao wanaotokea kijiji kilicho mashariki mwa jimbo la Orissa nchin India, walishikana kwenye kichwa hali inayofahamika kama craniopagus.

Craniopagus hukumba mtoto mmoja kati ya watoto milioni 3 wanaozaliwa na asilimia 50 ya wale wanaopatwa na hali hiyo hufariki saa 24 baada ya kuzaliwa.

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara