Manispa ya Temeke yaridhishwa na utekelezaji wa Miradi yake

                        Naibu Meya Manispaa ya Temeke Juma Rajab Mkenga

Halmashauri ya manispaa Temeke Jijini Dar es salaam kupitia kamati yake ya Maendeleo ya uchumi na fedha imeeleza kurudhishwa na hatua za utekelezaji wa miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mbali mabali ya manispaa hiyo.


Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo naibu  meya manispaa hiyo Juma Rajab Mkenga amesema kati ya miradi 5 inayotekelezwa minne ikiwemo ya Daraja, Zahanati, Shule na Soko inaendelea vizuri na kwamba kukamilika kwake itasaidia wakazi wa kata husika.

Hata hivyo licha ya kurudhishwa na baadhi ya miradi hiyo iliyofanyiwa ukaguzi, Naibu Meya Juma ameeleza kuwa kamati haikurudhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Sekondari ya Mbagala kuu kwa kile wanachodai ujenzi huo umechukua muda mrefu kuliko ilivyopangwa.

Kwa upande Diwani wa kata ya Kilungule huko Mbagala, Said Fella ameeleza kufurahishwa na hasa kukamilika kwa Zahanati ya Charambe kuwa anaamini kukamilika kwa miradi hiyo itawarahisishia na kupunguza kero kwa Wananchi.

Miradi iliyokaguliwa na kamati hiyo ni Ujenzi wa Daraja linalounganisha Mbagala Kijichi na Toangama, Ujenzi wa Zahanani ya Mbagala na Charambe, Ujenzi wa Sekondari ya Mbagala na Ujenzi wa soko la Buza.


Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara