Ligi kuu spania kuanza kutumia VAR Mwakani
Bosi wa shirikisho la soka nchini Hispania RFEF, Juan Luis Larrea amesema teknolojia ya Video Assistant Refaree (VAR) itaanza kutumika kwenye La Liga na Copa del Rey kuanzia msimu ujao.
“Tuna mpango wa kutekeleza matumizi ya VAR katika La Liga mwanzo wa msimu ujao”, amesema rais wa muda wa Royal Spanish Football Federation (RFEF) Juan Luis Larrea.
Ligi kuu ya Hispania ni moja ya ligi tano bora barani Ulaya ambazo hazitumii teknolojia ya usaidizi wa video, (VAR) ambayo itatumika rasmi kwa mara ya kwanza kwenye Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.Kwa upande wa Rais wa LaLiga, Javier Tebas amesema kuwa teknolojia hiyo ni ghali sana, lakini Larrea amesema RFEF ipo tayari kukubali mabadiliko hayo bila kujali gharama zake.
Aidha Larrea amesisitiza kuwa kuna teknolojia zinakuja kwenye soka na unapaswa kuzibali tu kwasababu zinasaidia kuondoa utata kwenye mchezo pendwa duniani.
Comments
Post a Comment