Kocha wa zamani wa simba anyakua ubingwa akiwa na Gor Mahia Kenya

Gor Mahia imeitwanga Kariobang Sharks kwa mabao 3-1 na kufanikiwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Kenya. Gor Mahia inanolewa kocha wa zamani wa Simba, Dylan Kerr imeshinda mechi hiyo leo na kukamilisha safari yake ya ubingwa msimu. Kerr ambaye ameichukua timu hiyo nusu msimu, amepata sare mbili, kapoteza moja na kushinda zilizobaki. Kerr amefanikiwa kuchukua ubingwa na Gor Mahia akiwa na mechi tatu mkononi. Mechi yake ya kwanza alipoteza kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam akicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Everton FC.

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara