Kocha wa timu ya Arsenal ajiuzulu
Pedro Martinez Losa amejiuzulu wadhfa wake wa klabu ya Arsenal upande wa wanawake baada ya miaka mitatu katika uongozi wa soka ya ligi ya wanawake.
Losa ambaye nia raia wa Uhispania, aliyewasili Septemba 2014 alikiongoza kikosi cha The Gunners 2016 kushinda kombe la FA mbali na kushinda kombe la kibara la WSL 2015.
Arsenal ambayo iko katika nafasi ya sita katika ligi wamejipatia pointi nne katika mechi zake tatu za kwanza katika msimu wa 2017-18.
''Pedro ametuongoza katika wakati muhimu wa mabadiliko na ametusaidia kuweka msingi wa mafanikio katika siku za usoni'', alisema afisa mkuu wa Arsenal Ivan Gazidis.
''Tunashukuru kwa kazi nzuri ya Pedro katika misimu mitatu iliopita''.
Comments
Post a Comment