Kikosi cha simba chaanza mazoezi rasmi Zanzibar kujiandaa na Yanga

Kikosi cha Simba kimetua mjini Zanzibar na kuanza kambi yake rasmi kuiwinda Yanga.

Simba inajiandaa katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa Simba chini ya Kocha Joseph Omog, wamepanga kuanza mazoezi magumu kesho asubuhi na watafanya mazoezi asubuhi na jioni kwa siku mbili mfululizo.

Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu kutokana na Simba na Yanga kulingana pointi, kila moja ikiwa na 15 na Simba ikiwa kileleni kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara