Joshua amshinda Mfaransa Zlatan ashuhudia Pambano

Bondia Carlos Takam kutoka Ufaransa ambaye alionekana kama sugu hivi, mwisho alishindwa kuvumilia ukali wa makonde ya Anthony Joshua katika raundi ya 10.

Joshua amemshinda Takam katika pambano la uzito wa juu kuwania mkanda wa IBF lililomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Cardiff.

Kabla Joshua alikuwa azichape na Kubrat Pulev lakini aliumia na kujitoa na Takam akachukua nafasi yake.


Ingawa alibezwa na wengi, Mfaransa huyo alionyesha kiwango kizuri na usugu licha ya kwamba Joshua alipiga ngumi nyingi zaidi.

Mabondia hao waligongana vichwa mapema kabisa, lakini walijitahidi kuendelea kupambana hadi raundi ya 10 Takam aliposhindwa.

Mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic alionyesha mapenzi yake kwa kumuunga mkono rafiki yake Joshua.


Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara