Iran:Tunaunda silaha yoyote kujilinda



Haki miliki ya pichaAFPImage captionRais Hassan Rouhani

Rais wa Iran amesema kuwa nchi yake itaunda silaha zozote inazohitaji kujilinda dhidi ya uvamizi.

Wakati akihubia bunge Rais Hassan Rouhani, alisema kuwa Iran haitakuwa ikikiuka makubaliano yoyote ya kimataifa kwa kuunda silaha yakiwemo makombora ya masafa marefu.

Aliionya Marekani kuwa ukiukaji wa mkataba wa nyuklia uliotiwa sahihi kati ya Iran na mataifa sita yenye nguvu ni kwa manufaa yake.

Rais wa Marekani Donald Trump hivi karibuni alikataa kuidhinisha mkataba huo akiitaja Iran kama nchi kaidi inayounga mkono ugaidi.

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara