IGP Sirro afanya ziara Kibiti na Ikwiriri Mkoani Pwani

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amesema kuwa  Jeshi hilo litaendelea kuwakamata na kuwachukulia hatua watu wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu pamoja na wanaojihusisha kuwafadhili wahalifu kutekeleza uhalifu

IGP Sirro amesema hayo akiwa Ikiwiriri mkoani Pwani kwa lengo la kuzungumza na wazee pamoja na viongozi wa kidini wa wilaya zote mbili za Kibiti na Ikwiriri, kutokana na ushirikiano walioupatia Jeshi hilo wakati wa kukabiliana na vitendo vya mauaji vilivyokuwa vikitekelezwa na watu wasiowaadilifu.

Aidha IGP Sirro amelipongeza Jeshi hilo kwa Operesheni zinazoendelea nchini hususan katika mkoa wa Mtwara, zilizofanikisha kukamatwa kwa milipuko 16, visu 97 pamoja na mbolea ya chumvi inayotumika kuchanganyia kutengeneza milipuko pamoja na watuhumiwa kadhaa.

Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi Liberatus Sabas, amesema katika operesheni zilizofanyika mkoani Mtwara, wamefanikiwa kuwakamata watu kadhaa wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu na kwamba operesheni kama hizo bado zinaendelea.

Akiwa mkoani Pwani, IGP Sirro, pia amewapandisha vyeo jumla ya askari 43 kutokana na kufanya kazi kwa kiwango cha juu huku akiwataka kuendelea kufanykazi zao kwa weledi katika kuwahudumia wananchi.

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara