Heche aikosoa Serikali

Mbunge wa Tarime  Vijiji, John Heche amekosoa uchaguzi mdogo wa marudio unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba na kusema kwamba fedha zinazotumika katika kufanya uchaguzi huo zingesaidia katika kuwapatia mikopo wanafunzi.

Mbunge Heche amelazimika kukosoa uchaguzi huo ambao Tume ya Uchaguzi imetangaza kwamba utafanyika mwezi Nov 26 katika Kata 43 huku kukiwa na madai ya kwamba kuna baadhi ya Madiwani walikuwa wamenunuliwa ili kuvihama vyama vyao.

Ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba  
"Mmetumia pesa kununua madiwani sasa mnatumia pesa za umma kufanya uchaguzi, pesa hizo zingetumika kuwapa mikopo wanafunzi wanaoteseka" Heche.

Mwanzoni mwa mwezi Oktoba,  Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza kuwa kutakuwepo kwa uchaguzi wa marudi mwezi Novemba  katika kata 43 ambazo madiwani wake walijiuzulu, wengine wakiwa wamefariki huku wengine wakiwa wametenguliwa na mahakama kwa kushindwa kuhudhuria vikao.

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara