Hatimaye Mfalme waThailand kuzikwa kesho

Mitaa ya Bangkok nchini Thailand imejazwa na watu wakiwa wamevalia makoti ya plastiki kuzuia mvua, kuwahi sehemu za kukaa ili kushuhudia na kumuaga kwa mara ya mwisho mpendwa wao ambaye alikuwa mfalme wa nchi hiyo Bhumibol Adulyadej.

Sherehe za kumuaga Mfalme huyo ambaye ameongoza Thailand kwa miaka 70 na kuwa kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi duniani zimechukua siku 5, ambapo hapo kesho inatarajiwa kuwa na umati mkubwa zaidi kwa kuwa mwili wa Mfalme Adulyadej utakuwa ukitolewa katika makazi ya kifalme na kupelekwa eneo la mazishi.

Mtoto wake wa kiume wa Mfalme Bhumibol Adulyadej ndiye anatarajiwa kuwasha moto ambao utachoma maiti ya baba yake, na kisha majivu yake kukusanywa na kurudishwa kwenye kasri ya kifalme siku ya Ijumaa, na kufuatiwa na sherehe nyingine kwa siku 2.

Bhumibol ambaye amefariki Oktoba13, 2016 akiwa na miaka 88, alikuwa mfalme mwenye kupendwa na wananchi wake na alijijengea heshima kubwa, mazishi yake yanatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa nchi za kifalme duniani na nyinginezo.

Mazishi hayo yamegharimu pesa ya Thailand bilioni 3, ambazo ni sawa na dola za Kimarekani milioni 90, na hapo kesho imetangazwa kuwa siku ya mapumziko kuruhusu raia wa nchi hiyo kupata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho, na pia askari wa jeshi la polisi 230,000 wa nchi hiyo watakuwa zamu kuangalia usalama.

Nchini Thailand wana utamaduni wakukaa na maiti ndani kwa muda mrefu, mwaka au zaidi kadri familia itakavyoamua, huku wakiendelea kuihudumia maiti hiyo kama mtu mgonjwa na kuzungumza nayo, na baadaye kuanza shughuli za mazishi.
Imetafsiriwa kutoka CNN na BBC.


Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara