Habari njema kwa wakazi wa Kigamboni Dar es salam
Baada ya ziara ya kamati ya huduma za jamii ya manispaa ya Kigamboni ikiongozwa na meya wake Maabadi Hoja kutembelea eneo maalumu litakalotumika kuuzia/ kununua magari Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Property International bwana Halim Zaharan ambao ndio wamiliki wa eneo hiloameendelea kusisitiza wawekezaji wajitokeze kwa wingi kwakuwa mpaka sasa wawekezaji 80 wameomba na kukubaliwa na eneo bado lipo na kwamba mji huo utakapo kamilika utakuwa umeenea kwa kila kitu.
Kuhusu makaazi ya wanachi, zimetengwa mita za mraba milioni moja na kwamba wananchi wasubirie bei elekezi ambayo itakuwa ni nifauu kulingana na maisha ya sasa.
Meya wa manispaa ya kigamboni Maabadi Hoja ameeleza kuridhishwa na kusudio la mradi huo na kwamba kukamilika kwake itaongeza pato sio tu kwa Kigamboni pekee bali kwa taifa, na mwisho ameshauri ujenzi wa miundombinu ya eneo hilo iende kwa kasi ili kuchagiza adhima hiyo.
Issa Zahoro ni diwani mkaazi wa kata ya kisarawe II ameeleza kuwa licha ya mradi huo kuwa na faida kubwa za kimaendeleo lakini kutakuwepo na fursa ya ajira kwa wananchi wa eneo hilo.
Comments
Post a Comment