Gigy Money ampa makavu Hemed Phd
Msanii Gigy Money ambaye hakauki vituko kwenye mitandao ya kijamii, amemjibu msanii mwenzake Hemedi Phd ambaye alisikika akimponda Gigy Money, na Gigy kurudisha mapigo akisema kwamba msanii huyo kwa sasa hayuko sawa kichwani kwani amezeeka. Gigy ameyasema hayo alipokuwa akiongea na mwandishi wa East Africa Television na kusema kwamba Hemedi yuko sawa aliposema hana hadhi ya kumzungumzia Gigy Money, kwani tayari msanii huyo hana pesa tena hata mawazo yake ni ya kizee, na ameshamsahau kama ni msanii. “Amesema yeye hana hadhi ya kumuongelea mtu kama mimi, mimi ndiyo simjui kwanza nimemsahau, nahisi sasa hivi atakuwa mzee sana na unajua watu wazee wanapotezaga akili na kumbukumbu, na kiukweli hawezi kuwa na hadhi ya kuniongelea mtu kama mimi kwa sababu hana hela, masikini”, amesema Gigy Money.
Comments
Post a Comment