CCM yaanza kuboresha viwanja vyake
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefunguka kuhusu mpango wake wa kuboresha viwanja vya mchezo wa soka nchini ambavyo vinamilikiwa na Chama hicho.
Akizungumza na eatv.tv leo, Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa CCM, Ndugu Humphrey Polepole amesema chama chake kimeanza maboresho viwanja vyake 22 nchini kote ili kukidhi vigezo vya soka ikiwemo kuwa na sehemu bora ya kuchezea (Pitch).
“Tumeanza maboresho makubwa kabisa ya viwanja vyetu tukianza na CCM Kirumba Mwanza pamoja na viwanja vingine kama Sheikh Abeid cha Arusha na Ally Hassan Mwinyi huko Tabora kwa kuweka nyasi orijino pamoja na maeneo ya ndani ya uwanja kama mabafu na vyoo”, amesema Polepole.
Aidha Polepole amesema serikali ya awamu ya tano imejipanga kuendelea kuboresha eneo la michezo kwa kushirikiana na shirikisho la soka nchini TFF ili kuweza kutengeneza ajira kwa vijana.
Comments
Post a Comment