Bayern Munich yamtolea njee Lewandowski

Baada ya mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski kusema anahitaji mshambuliaji mwingine ili kumpunguzia majukumu ndani ya klabu hiyo, mwenyekiti wa bodi ya timu Karl-Heinz Rummenigge amekataa.

Mwenyekiti wa bodi ya Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amesema haamini kama wanahitaji kusaini mshambuliaji mwingine kwaajili ya kumsaidia Robert Lewandowski.

Jumamosi hii mshambuliaji huyo raia wa Poland alipendekeza asajiliwe kwa mchezaji atakayesaidiana naye kwaajili ya kuipa klabu mafanikio kwasababu yeye kuna muda anachoka kutokana na timu kumhitaji kwenye kila mechi ya kila mashindano wanayoshiriki.

Rummenigge amesema bodi haina mpango wa kusajili mshambuliaji mwingine bali ataendelea kucheza Lewandowski labda awe na majeraha vinginevyo atacheza tu.

Pia bosi huyo wa Bayern ambaye pia aliwahi kuichezea timu hiyo amesema wanatambua wana majeruhi wengi katika kikosi chao hususani katika eneo la ushambuliaji na kocha anatambua hilo lakini anatumia wachezaji waliopo kuziba nafasi hizo.

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara