Alberto Msando afunguka
Wakili Maarufu Alberto Msando amefunguka na kusema kuwa anatamani baadhi ya vikundi vinavyoanzishwa kwa ajili ya maombi vipigwe marufuku kwani watu waonzisha vikundi hivyo wanalenga kujitafutia pesa na huku wananchi wa hali ya chini wakizidi kuumia.
Msando amesema hayo kupitia mtandao wake wa Instagram baada ya Nabii mmoja nchini Tanzania kuuandaa ibada ya maombi ya kuvunja laana ya kutembea kwa miguu huku akiwaahidi watu wote watakaofika kwenye misa hiyo watapata baraka na kupata magari na kusema magari yao yameshikiliwa na shetani baharini.
"Na kuna watu wataenda. Kuna watu wataamini masuala ya imani ni magumu sana ila kadri siku zinavyozidi kwenda haya mambo yanaongezeka. Hali ngumu ya maisha inasababisha baadhi ya watu kuamini kila kitu. Na wanaoanzisha hivi vikundi vya maombi wanafaidika sana. Ni wakati baadhi ya vikundi vipigwe marufuku" alisisitiza Msando
Comments
Post a Comment