Al Ahly dhidi ya Wydad Casablanca zatoka suluhu fainal za CAF

Fainali ya kwanza ya ligi ya mabingwa barani Afrika imefanyika jana kwenye uwanja wa Borg El Arab jijini Alexandria ikiwakutanisha wenyeji Al Ahly dhidi na Wydad Casablanca.

Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1 hivyo kufanya mchezo wa marudiano nchini Morocco kuwa na mvuto wa aina yake. Al Ahly walianza kuziona nyavu za Wydad kupitia kwa Moamen Zakaria ambaye alifunga kwa mkwaju mkali.

Wydad walisawazisha kupitia kwa Achraf  Bencharki hivyo kuwapa nafasi nzuri Wamorocco hao kuweza kutwaa ubingwa wao wa pili wa Afrika endapo watautumia vyema uwanja wa nyumbani wiki mbili zijazo.

Al Ahly ambao ni mabingwa wa kihistoria wa kombe hilo wakiwa wametwaa mara 8 watakuwa na wakati mgumu kutwaa ubingwa wa 9 nchini Morocco baada ya kushindwa kutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani.

Wydad Casablanca walitinga fainali kwa kuitoa USM Alger ya Algeria kwenye nusu fainali wakati Al Ahly waliitupa nje Etoile du Sahel.

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara