Ziwa Tanganyika lipo hatarini kupoteza samaki na dagaa kutokana na matumizi haramu ya uvuvi

Wadau wa sekta ya uvuvi katika Ziwa Tanganyika wamekubaliana kukomesha uvuvi haramu ambao unahatarisha kutoweka kwa samaki kutokana na matumizi ya sumu na nyavu zisizostahili katika kuvua ziwani humo. Makubaliano hayo yametokona na tafiti kadhaa kuonesha kuwa ziwa hilo la pili kwa kina kirefu duniani liko katika hatari ya kutoweka samaki na dagaa kutokana na matumizi haramu ya uvuvi. Wameshauri kuzingatiwa kwa sheria za uhifadhi zilizopo ili kila mmoja atimize wajibu wake. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia-Jenerali Mstaafu EMMANUEL MAGANGA amesema kila mmoja awajibike kuhakikisha uvuvi unakuwa endelevu pamoja na kuwaelimisha wananchi juu ya madhara ya uvuvi haramu.

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara