Simba yafanya mkutano mkuu

Kwa mara nyingine tena, Wanachama wa Klabu ya Simba wamekutana kufanya Mkutano Mkuu wa Klabu leo Jumapili kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyarere International Conference Centre) jijini Dar es Salaam. Ukumbi huo wa kisasa kabisa nchini upo maeneo ya Ocean Road, jirani na Chuo cha Usimamizi wa fedha (IFM), utakuwa unatumiwa kwa mara ya pili na klabu hiyo baada ya kutumika Jumapili iliyopita. Mkutano huo ni mwendelezo wa maandalizi ya Klabu ya Simba kufanya mabadiliko ya kimfumo katika kuiongoza klabu hiyo. Mmoja wa wanachama maarufu wa Simba, Mohamed Dewji ‘MO’ anatarajiwa kuwa mmoja wa wadau waliopanga kuwekeza baada ya mfumo wa uendeshaji kubadilishwa.

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara