Sierra Leone. Miili 500 yafukuliwa katika maporomoko ya ardhi

Waokoaji wamefukua miili 500 ya watu waliozikika katika maporomoko ya ardhi yaliyotokea maeneo karibu na mji muu wa Freetown nchini Sierra Leone wiki iliyopita . Janga hilo limesemekana kuwa baya zaidi barani Afrika kuwahi kutokea baada ya mlima Sugar Loaf kuanguka upande mmoja kufuatia mvua kubwa iliyonyesha . Watu 461 walifariki katika janga hilo na kadhaa bila kujulikana waliko . Siku ya Jumapili miili 500 ilipatikana na kuzikwa mara moja . Siku ya Ijumaa shirika la msalaba mwekundu lilifahamisha kuwa watu 600 walikuwa hawajulikani walipo .

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara