Kocha Ancelotti akatazwa kuvuta sigara

Kocha Ancelotti akatazwa kuvuta sigara MUUNGWANA BLOG / 2 hours ago Kocha wa FC Bayern Munich ya Ujerumani Carlo Ancelotti ni mmoja kati ya makocha ambao wanavuta sigara, Ancelotti amekuwa na utamaduni wa kupenda kuvuta sigara akiwa mazoezini, kitendo ambacho akimfurahishi mkurugenzi wa michezo wa Bayern. Leo August 18 Carlo Ancelotti ameambiwa na mkurugenzi wa michezo wa FC Bayern Hasan Salihamidzic kuacha kuvuta sigara akiwa maeneo ya club ya timu hiyo na mazoezini, maamuzi ambayo Ancelotti ameyakubali na ataachana na utamaduni huo. “Nimemuomba Ancelotti asiwe anavuta sigara akiwa club kiukuweli amekubali, Ancelotti ni professional” - Hasan Salihamidzic Kocha Carlo Ancelotti mwenye umri wa miaka 58 amewahi kukiri kuwa alianza kuvuta sigara toka akiwa na umri wa miaka 25 “Nilikuwa sivuti sigara katika maisha yangu sema nilijaribu siku moja, kwa sasa huwa navuta nikiwa nime-relax, baada ya dinner au ninapokuwa naangalia movie” - Carlo Ancelotti

Comments

Popular posts from this blog

Faida ya kutumia ganda la Ndizi mbivu

Kurudisha nguvu za kiume

HISTORIA: Ernesto Guevara