Posts

Wabungee acheni kuwashwawashwa na kufanya mambo ya umbea, Ndugai

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amesema kwamba hana taarifa za kujiuzulu kwa mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu , na wala hiyo barua bado haijamfikia, na kuita kitendo alichokifanya ni umbea. Job Ndugai ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio kwenye kipindi cha East Africa Breakfast, na kusema kwamba Lazaro hakupaswa kutangaza hivyo kabla ya kuhakikisha barua imemfikia. Pamoja na hayo Spika Ndugai amewataka wabunge wengine kuacha kuwashwa washwa na kufanya mambo ambayo ameyaita ni ya umbea.

Ndugai:Sina taarifa ya kujiuzulu Nyarandu

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amesema kwamba hana taarifa za kujiuzulu kwa mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu , na wala hiyo barua bado haijamfikia, na kuita kitendo alichokifanya ni umbea. Job Ndugai ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio kwenye kipindi cha East Africa Breakfast, na kusema kwamba Lazaro hakupaswa kutangaza hivyo kabla ya kuhakikisha barua imemfikia. Pamoja na hayo Spika Ndugai amewataka wabunge wengine kuacha kuwashwa washwa na kufanya mambo ambayo ameyaita ni ya umbea.

Polisi wawili wasimamishwa kazi

Image
Polisi wawili wa trafiki nchini Afrika Kusini wamesimamishwa kazi na wanakabiliwa na mashtaka ya kuaibisha kikosi cha polisi baada ya video yao "wakila pesa" kusambaa sana mitandao ya kijamii. Video hiyo inawaonesha polisi hao wawili wakitumia noti za pesa kuchonokoa meno yao na pia kujipangusa, huku muziki wa sauti ya juu ukisikika kwenye gari lao. Wawili hao wanaonekana pia wakila chakula chao cha mchana kutoka kwenye mikebe ya Styrofoam kwenye sehemu ya kubebea mizigo nyuma ya gari. Idara ya polisi wa jiji la Ekurhuleni amesema wafanyakazi hao, ambao wamevalia sare rasmi ya polisi wakati huo, wameiaibisha idara hiyo na kwamba vitendo hivyo si vya kistaarabu. Msemaji wa idara hiyo Wilfred Kgasago amesema wawili hao wamekabidhiwa barua za kuwasimamisha kazi mapema na kwamba watafika katika kamati ya nidhamu Jumanne. Waziri wa polisi nchini Afrika Kusini Fikile Mbalula alipakia video hiyo kwenye Twitter mwishoni mwa wiki, na akafurahia hali kwamba wawili hao wataadhibi...

Neymar aanza kuimisi Barcelona

Image
Hivi majuzi wikiendi Neymar alionekana nchini Hispania akirudi kuwasalimia washkaji zake wa Barcelona na kuonekana kupiga nao story nyingi sana hii ikiwa karibia mara ya tatu kwa Mbrazil huyo kurudi. Lakini wakati akiwa Hispania kumetoka ripoti toka Ufaransa kwamba Neymar hafurahii tena maisha ya PSG na Ufaransa kwa ujumla na ndio maana kila baada ya mechi huwa anaondoka nchini humo. Ugomvi kati ya Neymar na mshambuliaji mwenzake Edison Cavanni unatajwa kuwa moja kati ya sababu kubwa kwa Neymar kutopapenda PSG huku habari mpya zikidai Neymar hamfurahii kocha wa klabu hiyo. Neymar inasemekana kwamba hafurahii mbinu za kocha Unai Emery na inasemekana kocha huyo hapendwi na wachezaji wengi wa PSG kwani anawafanya wakose raha na kutojisikia amani PSG. Kingine kinachomfanya Neymar kujutia PSG ni habari kwamba wachezaji wenzake hawana furaha kutokana na upendeleo anaopewa na anamiss furaha aliyokuwa nayo akiwa na MSN wakati wa Barcelona.

Polisi wakamata vifaranga vya kuku 6,400

Image
Arusha. Vifaranga vya kuku 6,400 vinatarajiwa kuchomwa moto baada ya kunaswa vikiingizwa nchini kupitia Longido mkoani Arusha. Vifaranga hivyo vilikamatwa juzi vikitokea nchini Kenya. Taarifa zinasema thamani ya vifaranga hivyo ni Sh12.5 milioni na ni mali ya mfanyabiashara Mary Matia (23) mkazi wa Mianzini jijini Arusha anayeshikiliwa na polisi. Akizungumza na Mwananchi katika mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Namanga, ofisa mfawidhi wa Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa ya Mifugo Kanda ya Kaskazini, Obedi Nyasembwa alisema tangu mwaka 2007 Serikali ilipiga marufuku kuingiza mayai na vifaranga kutoka nje ya nchi. Alisema uamuzi huo wa Serikali ulichukuliwa ili kudhibiti magonjwa ya mifugo ukiwamo wa mafua ya ndege. “Kwa mujibu wa Sheria ya Magonjwa ya Wanyama ya mwaka 2003, vifaranga hivi tutaviteketeza kwa kuwa vinaweza kuwa na magonjwa,” alisema. Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika mpaka wa Namanga, Edwin Iwato alisema kwa mujibu wa sheria vifa...

Sweden kumwaga mabilioni

Image
BALOZI WA SWEDEN NCHINI, KATARINA RANGNITT. SWEDEN imetoa Sh. bilioni 80.4 kwa Umoja wa Mataifa (UN) ili kusaidia kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuhamasisha wanawake kushiriki katika siasa nchini. Fedha hizo pia zitaelekezwa katika kusaidia kukuza uchumi, upatikanaji wa ajira, kuimarisha utawala bora na usawa wa kijinsia. Katika hafla ya kutiliana saini jijini Dar es Salaam jana, Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt, alisema msaada huo kwa kiasi kikubwa utaelekezwa kusaidia masuala ya kimaendeleo kwenye maeneo yanayomgusa mwanamke. Alisema Sh. bilioni 33 zitatumika kuwasaidia wafanyabiashara wadogo ili kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hususani kwa wanawake na vijana wakati Sh. bilioni 22 zitatumika kwa ajili ya kuleta uwazi na uwajibikaji serikalini, kuimalisha shughuli za kibunge, haki za binadamu, kuwakinga waandishi wa habari na kuziinua redio ndogo zisizosikika ili wananchi wapate zaidi habari. Alisema Sh. bilioni 26.4 zitatumika kuwahama...

Yanga kumaliza hasira zao kwa Singida United

Image
KOCHA WA TIMU HIYO, GEORGE LWANDAMINA. BAADA ya kuambulia pointi moja dhidi ya Simba kwenye mechi iliyopita katika Uwanja wa Uhuru, Yanga itaondoka Dar es Salaam kesho kuelekea Singida ikiwa na hasira ya kukisambaratisha kikosi cha Hans van der Pluijm, Singida United. Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, kama ilivyo kwa Singida United na Simba, Jumamosi ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya watani zao hao wa jadi kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara. Kikosi hicho cha Yanga katika safari hiyo, kitaendelea kuikosa huduma ya wachezaji wake wa kigeni, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Thabani Kamusoko ambao bado hawajapona kwa asilimia 100. Akizungumza na Nipashe jana, kocha wa timu hiyo, George Lwandamina, alisema kuwa matokeo waliyoyapata dhidi ya Simba yamewapa ari ya kufanya vizuri kwenye mchezo wao huo wa ugenini. "Hatutakuwa na Tambwe, Ngoma na Kamusoko kama ilivyokuwa kwenye mchezo dhidi ya Simba, lakini hilo halinipi shida sana, nakiamini kiko...