Posts

Viongozi wawili wa Acacia wajiuzulu

Image
Dar es Salaam. Wakati utekelezaji wa makubalino baina ya Serikali na Barrick ukisubiriwa, Ofisa Mtendaji Mkuu na Ofisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya Acacia, wametangaza kujiuzulu kuanzia leo Alhamisi. Kwenye barua yake, Ofisa Mtendaji Mkuu, Brad Gordon amesema anataka kurudi nyumbani Australia kusimamia masuala ya familia yake wakati Ofisa Mkuu wa Fedha, Andrew Wray akisema amepata fursa nzuri zaidi sehemu nyingine. “Pamoja na uamuzi huo, wote wataendelea kuhudumu kwenye nafasi hizo wakati wakikabidhi majukumu ya ofisi kwa warithi wao,” imesema taarifa ya Acacia iliyotolewa leo Alhamisi asubuhi. Kuziba nafasi hizo, Bodi ya Wakurugenzi wa Acacia imemtangaza Peter Geleta kuchukua majukumu ya ofisa mtendaji mkuu baada ya Gordon na Jaco Maritz kusimamia masuala yote ya fedha za kampuni hiyo. Wote wawili walikuwa watendaji wa Acacia kwa muda mrefu. Geleta alikuwa mkuu wa oganaizesheni wakati Maritz alikuwa meneja mkuu wa idara ya fedha. “Licha ya majukumu ya uendeshaji...

Faida mbalimbali za Tangawizi katika mwili wa binadamu

Image
Hicho ni kiungo kinachotokana na mzizi wa mmea unaoitwa Tangawizi. Ni mmea unaofanana sana na binzari, ikiwa bado haijamenywa maganda yake. Pia, ni bidhaa inayopatikana nchi nzima kwa bei nafuu kabisa na kila mtu mwenye uwezo wowote wa kiuchumi, anaweza kununua aidha kwa kipande kimoja, fungu au hata kilo akipenda. Hivi karibuni akiwa mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, ambaye sasa ni mbunge wa Viti Maalum (CCM), aliendesha kampeni kubwa ya uzalishaji wa tangaweizi wilayani humo, ikiwa sehemu ya zao la biashara. Mmea huo unaweza kuonekana kama wa kawaida na watu kuutumia tu katika mtindo wa mazoea, lakini ni kiungo kinachotumiwa kama dawa. Pia, kiungo hicho kinaweza kutumika kikiwa ama kibichi au kimekaushwa na kutengenezwa katika mfumo wa unga. Faida zake Tangawizi ni kati ya mimea mingi yenye maajabu. Unaweza kutumika kama dawa na kutibu magonjwa zaidi ya 72 mwilini mwa mwanadamu. Ina faida zaidi hasa kwa wagonjwa walioathirika na maambukizi ya Ukimwi. Hivyo, kwa wale we...

Samata kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2017

Image
Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF imetaja orodha ya wachezaji 30, watakao wania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2017 huku jina la mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta anayecheza KRC Genk likiwemo katika  listi hiyo. Baadhi ya wachezaji waliyopo katika orodha ni pamoja na mshindi wa mwaka 2015, Pierre-Emerick Aubameyang, mshindi wa tatu mwaka 2016, Sadio Mane huku jina la mshindi wa mwaka jana, Riyad Mahrez raia wa Algeria likikosekana. Mbwana Samata (Tanzania & Genk), Vincent Aboubakar (Cameroon & Porto), Karim El Ahmadi (Morocco & Feyenoord), Christian Atsu (Ghana & Newcastle), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund), Eric Bailly (Cote d’Ivoire & Manchester United), Cedric Bakambu (DR Congo & Villareal), Keita Balde (Senegal & Monaco), Christian Bassogog (Cameroon & Henan Jianye), Yves Bissouma (Mali & Lille), Khalid Boutaib (Morocco & Yeni Malatyaspor), Yacine Brahimi (Algeria & Porto), Ess...

Mwamuzi Elly Sassi amjia juu manara

Image
Baada ya msemaji wa Simba Haji Manara jana kusema mwamuzi Elly Sassi aliwaonea kwenye mchezo dhidi ya watani wao wa jadi Yanga Novemba 28 mwamuzi huyo amejitokeza na kusema Haji Manara amekosa cha kuwaeleza Wanasimba. Elly Sassi amesema Haji Manara anatakiwa kujua sheria za soka kwanza ndio aongee vinginevyo aende TFF akapate mafunzo ya kuwa mwamuzi sio kuangalia tukio moja kisha kulitafsiri kiushabiki. “Nafikiri Haji Manara amekosa cha kuwaambia Wanasimba lakini matukio na maamuzi ya uwanjani siku ya mchezo hayana utata wowote kwa watu wanaojua sheria za soka ndio mana baada ya mchezo wakufunzi mbalimbali wa CAF walinipongeza”, amesema Elly Sassi. Mwamuzi huyo ambaye amejizolea sifa miaka ya hivi karibuni kutokana na uchezeshaji wake ameenda mbali zaidi na kutafsiri kisheria matukio ambayo Manara anahisi yalipaswa kuwa penalti. “Tukio la Yondani kisheria ni kweli alishika, lakini dhamira na namna ya tukio lilivyokuwa mkono haukuwa na mawasiliano na mpira na alik...

Jela miezi 6 kwa kuoa mke wa pili Pakistan

Image
Mahakama nchini Pakistan imemfunga mwanamume mmoja miezi sita jela ya kuoa mke wa pili bila ya idhini kutoka kwa mke wake. Mahakama hiyo ya mjini Lahore pia ilimuamrisha Shahzad Saqib, kulipa faini ya dola 1,900, na kukataa maoni yake kuwa dini ya kiislamu inamruhusu kuoa hadi wake wanne. Mke wa kwanza wa Sadiq Ayesha Bibi, alikuwa amefanikiwa kujitetea kuwa kuoa bila idhini yake ulikuwa ni ukiukaji wa sheria za familia nchini Pakistan. Wanaharakati wa masuala ya wanawake wabasema kuwa kesi hiyo ni pigo kwa ndoa za wake wengi. Mfasiri wa FBI afunga ndoa na mwajiri wa IS Pia walisema kuwa itawapa wanawake zaidi walio katika hali kama hizo motisha ya kupeleka kesi mahakamani. Nchini Pakistan, wanaume wanaotaka kuoa wanawake kadhaa hufanya hivyo baada ya miaka kadhaa na ni lazima wapate idhini kutoka kwa mke wa kwanza. Baraza la kiislamu nchini Pakistan ambalo hutoa ushauri wa serikali kuhusu masuala ya kiislamu, mara kwa mara limekosoa sheria za familia nchini humo. Sadiq ana h...

Watu 34 wahukumiwa kunyongwa

Image
Watu 34 wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, (Albino), ambapo matukio 67 ya ukatili dhidi ya albino yakiwa yameripotiwa. Takwimu hizo zimetolewa katika muendelezo wa mkakati wa kitaifa wa kupiga vita ukatili, mauaji na unyanyasaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi ambapo Wakili kutoka Ofisi Mkurugenzi wa Mashtaka, Beatrice Isembo, amesema, pamoja na adhabu za vifo, watuhumiwa 17 wamehukumiwa vifungo tofauti huku kesi nyingine zikiendelea. "Tumegundua mikoa ya kanda ya Ziwa ndiyo iliyoongoza kwa matukio ya aina hii  na yote ni kutokana na imani za kishiriki kama kutaka utajiri kwenye uvuvi, mazao nk." Mwanza inaongoza kwa kuwa na kesi za aina hii 15, na jumla ya matukio 67 yameripotiwa katika kipindi cha miaka 11" amesema Bi. Isembo. Kwa upande wake, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Ralph Meela, kutoka Makao Makuu ya jeshi la polisi Idara ya Upelelezi kitengo cha makosa dhidi ya binadamu na usalama barab...

Julio aanza majigambo

Image
KOCHA MKUU WA TIMU YA DODOMA FC YA DODOMA, JAMHURI KIHWELU ‘JULIO’,. KOCHA Mkuu wa timu ya Dodoma FC ya Dodoma, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, amesema matokeo mazuri ambayo timu yake inapata katika mechi za Ligi Daraja la Kwanza yanatokana na wao kujipanga na si kubebwa kama baadhi ya wadau wanavyosema. Akizungumza na gazeti hili jana, Julio, alisema kuwa anaamini kikosi chake kina nafasi ya kupanda daraja na kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao kwa sababu wamejipanga kuendelea kupambana ili watimize malengo waliyoyaweka. Beki na kocha huyo wa zamani wa Simba alisema pia ligi hiyo ni ngumu na ina changamoto mbalimbali huku akiweza wazi kukukutana na ushindani kwenye michezo yote wanayocheza. “Hakuna mechi rahisi, tunapambana katika kila mechi, hatubebwi, hata ukiangalia matokeo yetu, mechi nyingi tulizoshinda tumecheza ugenini, tutaendelea kupambana tutakaporudi kumalizika michezo ya nyumbani," alisema Julio. Baada ya juzi kupata ushindi wa mabao 2-1 ...